DAR ES SALAAM:TAMASHA LA GOSPEL HARMONY LAFANA
Waimbaji wote wakiimba wimbo wa pamoja |
Gospel Flames wakiimba na mwimbaji wa bass wa Vocapella |
Light Bearers |
Asha Majura akiimba |
Vocapella toka Temeke |
Mwimbaji wa Vocapella Daniel Mutani akiimba kwa hisia |
Kwaya ya Upendo Azania nayo ilikuwepo |
Mwimbaji toka nchini Uganda anayeishi nchini Kenya,Israel Mugisha aligusa nyoyo za watu |
Light Bearers wakiimba |
Mkurugenzi wa JCB Studioz Waziri Barnabas akitoa shukrani kwa waliohudhuria |
Mchungaji Baraka Butoke akitoa hotuba ya kufunga tamasha |
Kutoka kulia ni Felix Makachayo,watangazaji wa Morning Star Radio Manase Rusaka na Prince Emanueli |
Tamasha la Gospel Harmony lilifanyika jana juni 14 mwaka huu katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam huku waliohudhuria tamasha hilo wakishuhudia uimbaji mzuri toka kwa Vocapella,Light Bearers,Asha Majura,Mugisha Israel toka Kenya,Edina Matinde na Gospel Flames,Angel Magoti na Kwaya ya Upendo ya Azania.
Mkurugenzi wa JCB Studioz ambao ndo walikuwa miongoni mwa wadhamini wa Tamasha hilo Waziri Barnabas alikaririwa na blog hii jana kuwa ameamua kuwekeza katika muziki wa injili ili kuleta chachu ya maendeleo ya muziki wa kiadventista hapa nchini hii ikiwa ni shukrani kwake kwa Mungu kutokana na mambo ambayo Mungu amemtendea maisha na pia kuhakikisha muziki huo unakuwa wa viwango vya kimataifa.
Mmoja wa walimu wa nyimbo za Injili Felix Makachayo aliyekuwepo kwenye tamasha hilo ambalo pia lilikuwa nimedhaminiwa na mtangazaji blog,Gospel Flame Ministries,Sagati Graphics,alipongeza maandalizi ya tamasha hilo na waimbaji walivyowatendea haki watu waliokuwa wamehudhuria tamasha hilo na kuomba tamasha hilo liwe chachu kuwa na matamasha yaliyopangika na kuleta hamasa ya uimbaji nchini.
Post a Comment