MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:TAMASHA LA GOSPEL HARMONY LAFANA


Waimbaji wote wakiimba wimbo wa pamoja


Gospel Flames wakiimba na mwimbaji wa bass wa Vocapella




Light Bearers



Asha Majura akiimba

Vocapella toka Temeke


Mwimbaji wa Vocapella Daniel Mutani akiimba kwa hisia

Kwaya ya Upendo Azania nayo ilikuwepo


Mwimbaji toka nchini Uganda anayeishi nchini Kenya,Israel Mugisha aligusa nyoyo za watu


Light Bearers wakiimba

Mkurugenzi wa JCB Studioz Waziri Barnabas  akitoa shukrani kwa waliohudhuria


Mchungaji Baraka Butoke akitoa hotuba ya kufunga tamasha


Kutoka kulia ni Felix Makachayo,watangazaji wa Morning Star Radio Manase Rusaka na Prince Emanueli




Tamasha la Gospel Harmony lilifanyika jana juni 14 mwaka huu katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam huku waliohudhuria tamasha hilo wakishuhudia uimbaji mzuri toka kwa Vocapella,Light Bearers,Asha Majura,Mugisha Israel toka Kenya,Edina Matinde na Gospel Flames,Angel Magoti na Kwaya ya Upendo ya Azania. 

Mkurugenzi wa JCB Studioz ambao ndo walikuwa miongoni mwa wadhamini wa Tamasha hilo Waziri Barnabas alikaririwa na blog hii jana kuwa ameamua kuwekeza katika muziki wa injili ili kuleta chachu ya maendeleo ya muziki wa kiadventista hapa nchini hii ikiwa ni shukrani kwake kwa Mungu kutokana na mambo ambayo Mungu amemtendea maisha na pia kuhakikisha muziki huo unakuwa wa viwango vya kimataifa.

Mmoja wa walimu wa nyimbo za Injili Felix Makachayo aliyekuwepo kwenye tamasha hilo ambalo pia lilikuwa nimedhaminiwa na mtangazaji blog,Gospel Flame Ministries,Sagati Graphics,alipongeza maandalizi ya tamasha hilo na waimbaji walivyowatendea haki watu waliokuwa wamehudhuria tamasha hilo na kuomba tamasha hilo liwe chachu kuwa na matamasha yaliyopangika na kuleta hamasa ya uimbaji nchini.

3 comments

markseven.bloggsport.com said...
This comment has been removed by the author.
markseven.bloggsport.com said...

Matamasha ya aina hii ndio yanayo takiwa katika kukuza viwango vya uimbaji, ni vema kama tukaamka sasa na kuwa serius katika uandaaji wa matamasha yenye viwango kama hili, ili kuyafikia malengo. Niwashukuru sana wandaaji wa tamasha la Gospel harmony pamoja na waimbaji woote walio fanikisha mapinduzi haya ya matamasha ya uimbaji wa nyimbo za injili. Mungu awabariki sana na kuwaongezea ubunifu zaidi.

Unknown said...

inapendeza sana,Tamasha kama hizi ziendelee kuandaliwa zaidi.SDA Mungu kawabariki

Mtazamo News . Powered by Blogger.