MTANGAZAJI

WATAFUTANJIA WAADVENTISTA WAPATA AJALI

 


Ajali ya Basi iliyo husisha gari la  Klabu ya Wafutanjia ya Waadventista wa Sabato ya  Grand Prairie kutoka Alberta, Canada, imesababisha kifo cha kiongozi mmoja mzima na wengine kadhaa kujeruhiwa kisha kupelekwa hospitalini. 

Ajali hiyo ilitokea usiku wa Februari 7, mwaka huu wakati kikundi hicho kilipokuwa kinarudi nyumbani kutoka kwenye tukio la Shindano la usomaji wa Biblia kwa mwaka(PBE), kwa mujibu wa ujumbe uliosambazwa na Huduma za Klabu za Divisheni ya Amerika ya Kaskazini ya Kanisa la Waadventista wa Sabato (NAD). 

Viongozi wa kanisa wanasema kuwa wahudumu wa dharura walisafirisha wanachama na viongozi waliobaki wa klabu kwenda hospitali za karibu, ambapo wanapatiwa huduma za matibabu.

Katika taarifa iliyotolewa kwa idhini ya maafisa wa eneo hilo, Huduma za Klabu za watafutanjia wa NAD zilieleza tukio hilo kuwa la kusikitisha na kuhamasisha jamii ya kanisa kwa ujumla kuombea walioathirika. Ingawa maelezo kuhusu sababu ya ajali bado hayajafahamika kwa umma, viongozi walisema kuwa hali bado inachunguzwa.

 “Tafadhali ombeni kwa familia yetu ya Watafutanjia katika jimbo la Alberta wanapolia kutokana na msiba kiongozi,” ujumbe huo ulisema.

 Mchungaji  Dan Wilson wa Kanisa la Grand Prairie, ameandika kwenye wasifu wake wa Facebook "Dereva wa basi alijaribu kubadilisha njia karibu na kutoka DeBolt na alipoteza udhibiti kutokana na barafu kali. Basi liliviringita mara mbili, na watoto wetu na watu wazima wengi walitupwa nje. Giza na baridi, walijitahidi kadri ya uwezo wao kusaidia kila mmoja. Mmoja wa watoto wetu alipata simu na kupiga 911. Ninalia kwa moyo wangu wote kueleza kuwa Lillian Banda alifariki papo hapo baada ya kutupwa nje ya Basi"

Habari hii imesababisha mwitikio mkubwa wa msaada kutoka kwa waumini wa kiadventista kote Amerika ya Kaskazini, wengi wao wakiashiria huzuni na mshikamano na familia zilizoathirika. 

Viongozi wa kanisa walisema kuwa wataendelea kutoa taarifa zaidi kadri taarifa zinavyopatikana. Wakati huu, waliwahimiza kuendelea kuombea uponyaji na faraja kwa waliojeruhiwa, familia zinazolia, na jamii yote ya Watafutanjia ya Alberta.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.