TANZANIA YAENDELEA KUAGIZA SUKARI TOKA NCHI ZA NJE
Serikali ya Tanzania inalazimika
kuagiza tani 290,000 za sukari kila mwaka toka nchi za nje ili kufidia pengo la uzalishaji wa
sukari nchini humo.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa
Kilimo, Chakula na Ushirika nchini Tanzania Godfrey Zambi, ambapo anaeleza kuwa mahitaji ya sukari
nchini humo kwa mwaka ni wastani wa tani 590,000 huku tani 420,000 zikiwa ni kwa
ajili ya matumizi ya nyumbani na tani 170,000 za viwandani.
Taarifa ya waziri huyo inaonesha kuwa uzalishaji wa
sukari nchini Tanzania kwa mwaka ni wastani wa tani 300,000 ambazo ni kwa matumizi ya
nyumbani tu ambapo, msimu wa mwaka 2014/15, serikali iliidhinisha tani 100,000 tu za sukari ya matumizi ya kawaida
kuingizwa nchini humo kati ya Machi na Mei mwaka huu.
Tani 182,765 ziliidhinishwa kuingizwa
nchini kati ya Julai 2014 na Juni 2015 kwa ajili ya matumizi ya viwandani.
Naibu Waziri huyo amesema punguzo la
ushuru kwa sukari inayoingizwa nchini pamoja na kusaidia bei ya sukari
kupungua, imekuwa ikisaidia bei ya mlaji kutopanda.
Post a Comment