MKUTANO MKUU WA KANISA LA WAADVENTISTA ULIMWENGU (GC) KUTOFANYIKA MWAKA HUU
Kamati ya Utendaji ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni iliyoketi Machi 19 mwaka huu imeaihirisha Mkutano Mkuu wa Kanisa la Waadventista Ulimwenguni uliokuwa ufanyike Indiana nchini Marekani mwaka 2020 hadi Mei 2021.
Tovuti ya Makao Makuu ya Kanisa hilo imeeleza kuwa Kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika kwa njia ya teknolojia ya masafa inayowezeshwa na intaneti kimewahusisha wajumbe wake walioko katika nchi mbalimbali Duniani.
Uamuzi huo umepigiwa kura na kupitishwa na kikao hicho baada ya mapendekezo ya Machi 17,2020 yalitolewa na Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Kanisa hilo (ADCOM) kuahirisha Mkutano huo kwa muda wa miaka miwili kutokana na janga la ugonjwa wa Covid-19 lilozikumba nchi mbalimbali duniani.
Kikao hicho kimepitisha kuwa ni wajumbe tu ambao watahudhuria Mkutano Mkuu wa mwakani , hakutakuwa na mabanda ya taasis mbalimbali kama ilivyokuwa ikifanyika awali na kipindi cha Uongozi wa Kanisa hilo kitaendelea kama kawaida.
Mkutano Mkuu wa Kanisa hilo Ulimwenguni kwa mwaka 2021 umepangwa kufanyika Indianapolis, Indiana nchini Marekani Mei 20 hadi Mei 25,Awali ilikuwa ufanyike It was originally scheduled Juni 25 hadi July 4, 2020.
Janga la Ugonjwa wa Covid-19 limesambaa duniani toka mwaka 2019,Januari 30,Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuwa ugonjwa huo ni janga la Dunia,ambapo mpaka sasa virusi vya ugonjwa huo vimeathiri zaidi ya watu 230,000 huku zaidi ya vifo vya watu 9,300 wakitokana na ugonjwa huo.
Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni lenye makao yake Makuu
Post a Comment