MTANGAZAJI

AMBASSADORS OF CHRIST CHOIR TOKA RWANDA KUFANYA ZIARA NCHINI MAREKANI AGOSTI MWAKA HUU



Waimbaji wa Ambassadors of Christ toka Rwanda watafanya ziara yao ya kwanza nchini Marekani Agosti mwaka huu ambapo watahudumu kwa mkutano wa makambi na Mkutano wa Injili utaoendeshwa na Mwinjilisti wa Kimataifa Dkt Herry Muhando toka Tanzania.

Taarifa toka kwa uongozi wa kwaya hiyo toka Kigali zinaeleza kuwa takribani waimbaji 17 wa kwaya hiyo ndio wanaotarajiwa kusafiri kwenda nchini Marekani ambako watahudumu kuanzia Agosti 4 hadi 18 mwaka huu katika miji ya Dallas na Huston katika mkutano wa Injili na kufanya tamasha la Uimbaji kwa Ushirikiano na waimbaji wa Kiadventista walioko katika maeneo hayo.

2 comments

Anonymous said...

Nunua tikiti hapa https://www.eventbrite.com/o/mount-zion-fellowship-17474566665

Anonymous said...

Futua @mountzionfellowship on Facebook kupata tikiti

Mtazamo News . Powered by Blogger.