MAHABUSU KADHAA ARUSHA WAGOMA KULA ILI KESI ZAO ZISIKILIZWE
Mahabusu
kadhaa walioko katika gereza kuu la Arusha wanaotuhumiwa kwa makosa ya
kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi na mirungi imeelezwa kuwa afya zao
zimezorota kutokana na kugoma kula chakula kwa kipindi kirefu ili kushinikiza
vyombo husika kusikiliza kesi zao.
Baadhi ya mahabusu hao ambao
waliweza kuzungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufikishwa katika mahakama kuu jijini Arusha jana walieleza
kuwa hali hiyo inatokana na kesi zao kukaa kwa muda mrefu bila
kusikilizwa,baadhi yao kesi zikiwa na zaidi ya miaka miwili bila
kusikilizwa jambo ambalo limewafanya kuonyesha hisia zao kwa njia ya mgomo wa kula
chakula katika kushinikiza vyombo husika kusikiliza kesi zao ili kubaini wana
hatia ama la.
Mwandishi wa habari hii ilishuhudia mahakamani hapo kwa kuwaona
mahabusu hao wakigoma kushuka kutoka kwenye karandinga lililokuwa limewaleta
mahakamani hapo.Hata hivyo baada ya muda mrefu baadhi yao walianza kushuka
katika basi hilo na hii ni baada ya kubembelezwa kwa muda mrefu.
Baada ya tukio hilo Mwandishi wa habari hizi alimtafuta msajili wa mahakama wa kanda ya kaskazini ndugu Mashauri
ambaye hakuwepo mahakamani hapo na alipozungumza kwa simu alisema yuko nje ya
mahakama hiyo Karatu kikazi hivyo hana
Taarifa juu ya mgomo huo Nakuahidi
kufuatilia swala hilo.
Post a Comment