MVUA ZAKATA MAWASILIANO KYELA,MBEYA
Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha
zimekata mawasiliano yanayoziunganisha barabara za Kyela Mjini na
Ipinda,Ipyana, Katumbasongwe, Bujombe,Bandari ya Kiwira Kasumulu,Kyela na
Ibungu, baada ya daraja la watembea kwa
miguu kusombwa na maji.
Tathmini ya awali iliyotelewa na
uongozi wa wilaya kwa mbunge wa kyela Dk
Harrison Mwakyembe inaonesha kuwa kata 11 kati ya 20 za wilaya
hiyo,zimeathirika na mafuriko,huku kata mbili za Bujonde na Kajunjumele zikiathirika
kwa kiwango kikubwa zaidi.
Mafuriko hayo pia yamesababisha vifo
vya watu watatu,huku wengine watatu, hawajulikani waliko,zaidi ya kata 60
hazina makazi baada ya nyumba zao kukumbwa na mafuriko na sasa wamejihifadhi
kwenye majengo ya shule zilizosalimika.
Waathirika wa mafuriko hayo
wanahitaji msaada wa haraka wa chakula,mavazi na malazi huku Baadhi ya wakazi
wa kyela wanasema kuwa mafuriko hayo ni makubwa kuzidi ya mwaka 1952 na
yale ya mwaka 1978.
Post a Comment