UTAFITI: WATOTO 800 WALILAWITIWA TANZANIA MWAKA 2013
Ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za binadamu nchini Tanzania imesema watoto wapatao 800 walilawitiwa nchini humo mwaka 2013.
Akiongea na BBC Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Dr Helen Kijo-Bisimba, amesema watoto wamekuwa katika maisha ya hatari Zaidi nchini humo kutokana na watu wa karibu wakiwemo wazazi wa kiume na hata kaka na wajomba zao kubainika wanawafanyia vitendo vya ubakaji.
Ripoti hiyo ambayo ni ya 11 kutolewa na taasisi hiyo imebainisha kuwepo kwa matukio ya raia kuwaua raia wenzao ambayo yameongeza kasi za ukiukwaji wa haki za kuishi nchini humo.
Aidha utafiti huo umeonyesha kuwa watu zaidi ya 1600 wakiwemo askari polisi wanane, waliuawa na wananchi wenye hasira kali katika matukio tofauti, huku askari polisi nao waliwaua raia 28 katika kipindi cha mwaka 2013.
Chanzo:BBC
Post a Comment