MTANGAZAJI

WAADVENTISTA WA SABATO TABORA WACHANGIA DAMU

Idara ya vijana ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato mkoani tabora wamechangia damu kiasi cha lita 80 katika mpango wa taifa wa damu salama kanda ya magharibi.

Uchangiaji huo umefanyika katika viwanja vya kanisa la waadventista wasabato kitete mjini tabora katika kutenda matendo ya huruma kwa kutoa misaada mbalimbali kwa wahitaji.

Naye mfanyakazi wa benki ya damu kanda ya magharibi Zaituni Abdallah amesema kuwa kumekuwa na mwitikio mkubwa wa waumini wa kanisa hilo kujitokeza kwa wingi kuchangia damu salama.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Vijana wa Unioni Konferensi ya Kaskazini Mch Elias Kasika amesema kuwa lengo la kutoa damu hiyo ni kuwasaidia wagonjwa walio hospitalini walio na ukosefu wa damu.


Kwa upande wake mratibu wa programu hiyo Daniel Ahmed amesema zoezi hilo litakuwa endelevu ili kuokoa maisha ya wananchi wenye maisha duni na kushindwa kupata damu kutokana na gharama.


Mwenyekiti wa vijana wa kanisa hilo la Kitete Michael Kigombe amewataka watanzania kujenga tabia ya kuwasaidia watu walio na maisha duni na katika kufanya hivyo wataokoa maisha yao

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.