MTANGAZAJI

HATIMAYE JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA AWASILISHA RASIMU YA KATIBA


 
Jaji Joseph Warioba


Hatimaye Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba leo amewasilisha Rasimu ya katiba mpya kwa wajumbe wa bunge maalum la katiba bungeni mjini Dodoma.

Uwakilishaji wa rasimu hiyo umefanyika leo baada ya mwenyekiti wa bunge hilo maalum hapo jana kuhirisha kikao hicho.


Miongoni mwa mambo yaliyowasilishwa ni pamoja na tunu za taifa ikiwemo muungano eneo lote la bara na visiwani ikiwemo miti na bahari.


Jaji warioba amesema kuwa yapo mapendekezo mengine ikiwemo kutunza historia ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na kuboresha misingi mikuu ya taifa ikiwa ni pamoja na kulinda misingi ya maadili ya nchi yoyote ile au jamii yoyote katika kutoa maamuzi.


Aidha jaji mstaafu Joseph warioba ameongeza kuwa wananchi walipendekeza wabunge wasiwe mawaziri ili kuwa karibu na wananchi wao huku wakisema kikomo chao katika ubunge kiwe awamu tatu na kusiwepo uchaguzi mdogo ili kuiepushia serikali gharama zisizokuwa za lazima.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.