DEOGRATIUS KIDUDUYE HATUKO NAYE
Mpaka mauti yanamkuta Kiduduye alikuwa ni mtangazaji katika kituo cha Radio Uhuru cha jijini Dar es salaam,nitaendelea kumkumbuka sana mwanahabari huyu kwa ushauri aliokuwa akinipa hasa kutokana na masuala ya utangazaji.
June 2007 Mimi na Marehemu Kiduduye tulibahatika kuhudhuria mafunzo ya wiki mbili ya uandishi wa habari huko Lusaka,Zambia.Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na NSJ ambayo yalihusu "Communication for Social Change"na kufanyika katika Hotel ya Longacres yaliwakutanisha waandishi wa habari 14 toka nchi za Tanzania,Zambia,Malawi,Lesotho,Botswana,DRC,Msumbiji na Zimbabwe. Nakumbuka tukiwa Zambia huko alininiuliza swali moja "je unafahamu Tanzania ilivyouzwa? na akanionesha email aliyokuwa ametumiwa iliyokuwa na orodha ya majina ya watu "walichota" pesa za walalahoi ambao miongoni mwao hivi sasa wanatuhumiwa kuwa ni MAFISADI. Huyo ndo Kiduduye ambaye amelala usingizi wa mauti.
Post a Comment