SAJENTI WA JESHI AWAPIGA RISASI WANAJESHI
Asubuhi ya Julai 6 mwaka huu, tukio la kusikitisha limetokea katika moja ya kambi kubwa za jeshi ya Fort Stewart , Marekani iliyopo jimboni Georgia, ambapo mwanajeshi mmoja ameripotiwa kuwafyatulia risasi wanajeshi wenzake watano.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka jeshi la Marekani, tukio hilo lilitokea majira ya saa 4:56 asubuhi kwa saa za Marekani, katika eneo la kitengo cha jeshi la Marekani kinachojumuisha vikosi vya wanajeshi wenye silaha nzito. Kambi hiyo iliwekwa chini ya ulinzi mkali muda mfupi baada ya tukio, na mshukiwa, ambaye ni Sajenti Quornelius Radford, mwenye umri wa miaka 28, alikamatwa ndani ya dakika thelathini na tano na wenzake waliomdhibiti kabla ya polisi wa kijeshi kufika.
Wanajeshi watano walijeruhiwa na kupatiwa matibabu katika hospitali ya Jeshi ya Winn na hospitali ya rufaa mjini Savannah. Taarifa kutoka kwa madaktari zinasema kuwa hali zao ni thabiti na wote wanatarajiwa kupona, huku watatu kati yao wakifanyiwa upasuaji.
Inadaiwa kuwa sajenti huyo alitumia bunduki ya binafsi, ambayo si sehemu ya silaha rasmi za kijeshi. Rekodi za jeshi zilizotolewa kwa vyombo vya habari zinaonyesha Radford aliingia jeshi Januari 2018. Alifanya kazi kwa cheo cha Sajenti wa usambazaji na hajawahi kutumwa kwenye vita.
Radford alikuwa na kesi ya kusikizwa Agosti 20 mwaka huu, mjini Hinesville, mji mdogo karibu na kambi, akikabiliwa na mashtaka ya kuendesha gari akiwa na pombe na kupita taa nyekundu baada ya saa moja asubuhi Mei 18 mwaka huu, kulingana na hati za mahakama. Alifanya kipimo cha damu na kuachiliwa kwa dhamana ya dola 1,818.
Mwanasheria Sneh Patel anayemwakilisha Radford katika kesi ya usafiri, lakini si katika tukio la risasi kama alivyosema Jumatano kupitia barua pepe. Alieleza kuwa hawezi kutoa maoni kuhusu mazungumzo yake na Radford kwa sababu ya siri ya mteja na wakili.
Mamlaka ya kijeshi ikishirikiana na shirika la upelelezi la FBI, wanaendelea na uchunguzi. Hadi sasa, sababu ya tukio hilo haijafahamika. Hata hivyo, tukio hili limeibua mjadala kuhusu sera za silaha binafsi katika kambi za kijeshi, kwani kwa kawaida, wanajeshi wa Marekani hawaruhusiwi kubeba silaha za binafsi bila kibali rasmi.
Post a Comment