WAADVENTISTA WAFANYA TAMASHA LA FILAMU
Kanisa la Waadventista wa Sabato katika Unioni ya Mashariki mwa Venezuela hivi karibuni lilifanya tamasha la filamu katika eneo hilo ambapo mamia walikusanyika kutazama zaidi ya filamu fupi fupi za kiinjilisti na kusherehekea utayarishaji wake.
Tukio hilo lilifanyika hivi karibuni katika Kituo cha Hifadhi ya Utamaduni huko Caracas, Venezuela.
Hernavid Torres, Mkurugenzi wa filamu wa Unioni ya Mashariki mwa Venezuela amesema wanavunja dhana potovu na filamu hizo zilizotayarishwa na timu yao ya vyombo vya habari vilivyoko katika Konferensi nane na field za unioni hiyo.
Tamasha hilo la filamu kwa muundo wa sinema linaloitwa UVOFilms, linakuwa la kwanza kuangazia filamu fupi fupi 16 zenye maudhui ya mafundisho ya Yesu.
Unioni hiyo ilifanya tamasha lake la kwanza la filamu mnamo mwaka 2019 kwa kiwango kidogo.
Ilikuwa muhimu kufanya tamasha la filamu ili kuwasilisha ujumbe wa wokovu kwa njia tofauti, anasema Lenny Hernández, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika Unioni ya Mashariki mwa Venezuela.
Zaidi ya waandishi 130 wa filamu, waigizaji, wapiga picha za video,wahariri, waliunda timu mbalimbali za utayarishaji ambazo ziliangazia fumbo moja katika nyanja tatu, filamu fupi, hali halisi au mtindo wa vipande vya video visivyozidi dakika 6:30.
Post a Comment