TIMU YA WAADVENTISTA YASHINDA KESI
Kesi iliyofunguliwa na Shule ya Waadventista ya Oakwood (OAA) dhidi ya Chama cha Riadha cha Shule za Sekondari cha Alabama (AHSSA) imetatuliwa mnamo hivi karibuni kwa uamuzi kwamba AHSSA itapanga siku mbadala kwa timu za michezo za Waadventista au kikundi kingine chochote cha kidini ambacho kinaweza kupinga kucheza kwenye mchezo ambao ni siku ya ibada.
Kesi hiyo ilifunguliwa dhidi ya AHSSA msimu huu wa masika uliopita, baada ya timu ya mpira wa kikapu ya OAA kufika katika nusu fainali ya mashindano ya serikali mwezi Februari, na kupoteza mchezo wao ulipangwa kuchezwa saa za Sabato.
Wakati timu zingine tatu kwenye mashindano zilikubali kubadilisha saa zao za mchezo ili kuendana na OAA, ombi hilo lilikataliwa na AHSSA, hata baada ya maombi kadhaa.
Gavana wa Alabama, Kay Ivey amepongeza uamuzi wa timu ya mpira wa kikapu ya Oakwood kusimama kwa imani yao, na akaandika barua kwa Chama cha Riadha cha Shule za Sekondari cha Alabama, akiomba majibu kwa nini hawakuweza kutimiza hitaji la OAA, haswa ikizingatiwa kuwa Chama cha Riadha cha Wanafunzi nchini Marekani NCAA tayari kinatambua wanafunzi wanaotunza Sabato na kuweka shule katika ngazi ya Chuo katika mashindano ya kitaifa.
AHSSA ilikubali kuzingatia sheria mpya, kuruhusu timu yoyote kuwasilisha siku ambazo inapinga kucheza kwa madhumuni ya kidini, mradi tu ziwasilishwe kabla ya muhula wa mwaka wa shule.
Todd McFarland, Naibu Wakili Mkuu wa Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista Ulimwenguni (GC),amefurahishwa na uamuzi huo. Ambapo amesema wanafurahi sana kwamba AHSAA ilifanya jambo sahihi.
Post a Comment