MTANGAZAJI

WANAZUONI WAJADILI UTAMBULISHO WA WAADVENTISTA WA SABATO

 


Hivi karibuni Chuo Kikuu cha Andrews (AU),ambacho ni Taasisi ya Waadventista wa Sabato huko Berrien Springs, Michigan, Marekani, kiliandaa mkutano uliojikita katika mada ya  Utambulisho wa Waadventista katika Historia na Theolojia.
Tukio hilo liliwaleta pamoja zaidi ya wanazuoni 30 kwa mazungumzo ya imani mbalimbali kuhusu utambulisho wa Waadventista.
Mkutano huo ulifadhiliwa na Ofisi ya Kumbukumbu, Takwimu, na Utafiti (ASTR) kwa ushirikiano na Taasisi ya Utafiti wa Kibiblia (BRI), Kitengo cha Machapisho ya Mama Ellen G. White, na Idara ya Historia ya Kanisa katika Seminari ya Theolojia ya Waadventista wa Sabato  ya Chuo Kikuu cha Andrews.
David Trim, Mkurugenzi wa ASTR na mwandaaji  mwenza wa mkutano huo, alibainisha, “Mazungumzo kuhusu utambulisho wa Waadventista daima yatakuwa muhimu kwa sababu kuna mwelekeo miongoni mwa makanisa ya Kikristo kutoweka pole pole 'kuyumba kwa utume' na kupoteza mwelekeo na shauku yao ya awali. 
Hivi sasa ni muhimu hasa kwa kongamano la utambulisho wa Waadventista kwani kanisa linakua kwa kasi katika sehemu mbalimbali ulimwengu.Ukuaji wa haraka waweza kuja na  hatari ya mabadiliko katika utambulisho,Ni muhimu kuzungumza juu ya kile ambacho kinatufanya tuwe Waadventista wa Sabato, na kisha tushiriki hilo na kanisa lote ulimwengu.
Rais wa Chuo Kikuu cha Andrews Andrea Luxton anasema hisia wazi ya utambulisho ndio huwapatia umakini na huwezesha kuwa na umoja ambapo ameongeza kuwa Inafaa haswa leo kwani tuko katika wakati wa mgawanyiko ulimwenguni. Ni rahisi kwa hilo kutuathiri katika kanisa.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.