WAADVENTISTA KUTOKA AFRIKA WASHIRIKI MAKAMBI KANSAS
Kundi la Waumini Waadventista kutoka Afrika wapatao 150 wamekuwa wakihudhuria katika ibada ya mara kwa mara kwenye Kanisa la Waadventista wa Sabato la New Haven huko Overland Park, Kansas, Marekani.
Kundi hilo lilianza mwaka wa 2003 kikiwa na familia na marafiki wachache kutoka Kenya ambao walikusanyika katika nyumba zao ili kujifunza Biblia na kuabudu ambapo Walitumia zaidi lugha ya Kiswahili wakati wa mikutano yao.
Kundi hilo tangu wakati huo limekua likijumuisha washiriki kutoka nchi nyingine za Afrika ikiwa ni pamoja na Tanzania, Ghana, Zimbabwe, Zambia, na Nigeria.
Mnamo 2017, Ezra Okioma, Mchungaji msaidizi katika Mtaa wa Wichita Kusini huko Kansas, alipewa jukumu la kuongoza kundi hilo.
Kundi hilo tangu wakati huo limendelea kukua kwa kiasi kikubwa, na kujitolea kwa Mch Okioma kutoa mafunzo na kuwawezesha viongozi wake. Usaidizi wa wachungaji wengine wa ndani katika Kanisa la New Haven pia umesaidia katika ukuaji na ushiriki wa washiriki wa jumuiya ya Kiafrika katika kanisa hilo.
Wakati wa janga la Uviko-19, kundi lilipata wanachama zaidi kupitia mikutano ya kawaida ya mtandaoni ambapo lilifanya Mkutano wa kwanza wa makambi ya mtandaoni ulifanyika Mei 2020 na zaidi ya washiriki 200 walihudhuria kupitia Zoom na watu watatu walijitoa kubatizwa.
Mkutano wa pili wa makambi ulifanyika mnamo Agosti 2021. Kundi lilifanya mkutano huo mtandaoni ambapo washiriki walihudhuria juma zima ,siku ya Sabato walihudhuria mkutano huo Kanisani.
Wakati wa mkutano mafundisho kuhusu afya, unabii, maisha ya familia, ujana, watoto yalitolewa huku watu zaidi ya 240 wakishiriki kwa njia ya Zoom kwa jumazima nzima,ambapo siku ya Sabato, zaidi ya watu 170 walihudhuria ana kwa ana na wengine wawili walibatizwa kutokana na mkutano huo.
Mwaka 2022, Kundi pia lilifanya mkutano wa makambi ya mseto, ambapo zaidi ya washiriki 300 walihudhuria kwa juma nzima. Siku ya Sabato, kundi lilikutana katika kanisa la Waadventista wa New Haven pamoja na washiriki wengine wa kawaida wa kanisa hilo . Zaidi ya waumini 250 wa kutoka afrika walihudhuria.
Post a Comment