MTANGAZAJI

AFISA WA ZAMANI WA SERIKALI YA NIGERIA AHUKUMIWA KIFUNGO MAREKANI

 

Afisa wa zamani wa serikali ya Nigeria amehukumiwa Jumatatu kifungo cha miaka mitano jela kwa kuiba zaidi ya dola za kimarekani  500,000 za misaada ya kukabiliana na janga la Corona nchini Marekani.

Abidemi Rufai alikuwa amevalia saa ya $10,000 na cheni ya dhahabu ya $35,000 alipokamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JFK mjini New York akielekea Nigeria Mei 2021.

Rufai alikiri hatia katika Mahakama ya Wilaya ya Tacoma, Washington, mwezi Mei ya kuwasilisha mashtaka ya ulaghai na wizi wa utambulisho uliokithiri, na Jaji Benjamin Settle alitoa hukumu hiyo Jumatatu. Hakimu pia aliamuru Rufai kulipa zaidi ya dola 600,000 kama marejesho.

Waendesha mashtaka walieleza kuwa  kijana huyo mwenye umri wa miaka 45 alikuwa na historia ya kulaghai serikali ya Marekani, ikiwa ni pamoja na kutumia vitambulisho vilivyoibiwa ili kuwasilisha msaada wa dharura baada ya vimbunga huko Texas na Florida.

Udanganyifu kama huo ulikuwa mkubwa katika mipango ya misaada ya janga la Corona , kwa mujibu wa Mkaguzi Mkuu wa Idara ya Kazi ya Marekani, ambaye alisema wiki iliyopita kwamba dola bilioni 45.6 zinaweza kuwa ziliipwa kimakosa katika bima ya ukosefu wa ajira kutoka Machi 2020 hadi Aprili 2022.

Idara ya Sheria ilifungua mashtaka dhidi ya watu kadhaa huko Minnesota juma lililopita kuhusu  na mpango wa udanganyifu wa dola milioni 250 ambao ulitumia mpango wa lishe ya watoto unaofadhiliwa na serikali wakati wa janga hilo.

Rufai, anayetoka  Lekki, Nigeria, ana shahada ya uzamili na ana uhusiano wa kisiasa katika nchi yake, waendesha mashtaka walisema. Alidaiwa kuwa anaendesha kampuni ya michezo ya kamari tangu 2016, fedha zake hazikuwa wazi na chanzo chake kikuu  cha mapato kinadaiwa kuwa ni kulaghai serikali ya Marekani.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.