MTANGAZAJI

VIJANA MEXICO WAPATA MAFUNZO YA UINJILISTI WA KIDIJITALI

 



Kanisa la Wa Adventista wa Sabato huko Chiapas, Mexico, lina nia thabiti ya kutoa fursa kwa mamia ya vijana wote katika eneo hilo kuwa wainjilisti wa kidijitali.
Wakati wa mafunzo ya hivi karibuni  ya mawasiliano, zaidi ya vijana 800 kutoka mamia ya makanisa ya ndani walikusanyika ili kuunda au kuboresha huduma zao za kidijitali kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii ili kueneza ujumbe wa injili.
Mafunzo hayo ya siku saba yalishuhudia mamia ya vijana wakikusanyika katika maeneo matano tofauti kote Chiapas hivi karibuni, ili kujifunza jinsi ya kuwa wanafunzi wabunifu wakati wa kutengeneza filamu fupi, kupiga picha na video kwa kutumia simu zao mahiri, kuandika habari na mengine mengi. Viongozi wa Kanisa waliiita ziara ya Mafunzo ya Mawasiliano na Matumaini.
Daniel Torreblanca, mkurugenzi wa mawasiliano na mkurugenzi wa huduma za vijana katika kanisa la Chiapas, amesema : "Ziara hii ya mafunzo ilikuwa muhimu sana kwa sababu wanataka vizazi vipya vihusike kumshirikisha Yesu na yale ambayo huwa ya kawaida kwao huku akisisitiza kuwa vijana wanajua zaidi kuhusu teknolojia kuliko vile tunavyoweza kufikiria na ingawa wengi hawakuwa na zana za hivi punde zaidi za kushiriki injili kwa ufanisi, kulikuwa na utayari wa kuvutia wa kujifunza miongoni mwao.
Vijana waliandika maelezo katika kila wasilisho na kuonyesha utayari wa kutumia karama na talanta zao kumtumikia Mungu.
Carlos Florentino, ambaye ni mfanyabishara karibu  na mpaka wa Mexico na Guatemala, alisafiri mamia ya kilomita kukutana Palenque kwa mafunzo hayo,yeye husambaza ujumbe wa matumaini na wafuasi wake 700 kwenye Facebook. Wakati wa juhudi za uinjilisti kanisani kwake, anashiriki mahubiri na ujumbe za kiroho kutoka kwa simu yake ya mkononi.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.