MTANGAZAJI

HOPE MEDIA HISPANIA YAPATA TUZO YA UZALISHAJI WA SANTURI BORA

 


Hope Media nchini Hispania imepokea Tuzo ya  ARPA kutokana na kuzalisha kwa Santuri  Bora ya nyimbo za Watoto nchini humo 
Utoaji wa tuzo hizo uliofanyika hivi karibuni na kuhusisha vyombo vya habari 30  katika ukumbi wa michezo maarufu wa "El Cantoral" huko Mexico City, hafla ambayo huandaliwa na  Chuo cha Taifa cha Muziki na Sanaa ya Kikristo (ANMAC), iliwakutanisha  na wanamuziki, wazalishaji wa nyimbo, wahandisi, na wataalamu wengine wa ubunifu wanaofanya kazi Mexico na Marekani.
Tuzo za ARPA ni utambuzi wa kimataifa wa sifa ya  kisanii na kiufundi ya aina ya muziki wa Kikristo wa lugha ya kihispaniola ambapo washindi wake hutokana na kura za wanachama waa ANMAC.
Lengo la tuzo za ARPA ni kutambua ubora na kuweka maanani kwa ulimwengu kwa muziki wa Kikristo na ujumbe wa kuokoa wa Bwana  Yesu Kristo.
Mchungaji Samuel Gil, mkurugenzi wa Hope Media Hispania, alipokea tuzo hiyo baada ya kuteuliwa katika vikundi vya "Matoleo ya Mwaka " na "Santuri  bora ya watoto," Hii ni mara ya kwanza kwa Kanisa la Wa Adventista wa Sabato Barani Ulaya kushinda tuzo hiyo katika kipengele hicho.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.