MTANGAZAJI

KONGAMANO LA VIJANA WA ADVENTISTA BARANI ULAYA

 


Tukio lililosubiriwa kwa muda mrefu limepangwa kuunganisha maelfu ya vijana wa Wa Adventista wa Sabato kutoka kote barani  Ulaya huko Lahti, Finland, Agosti 2-6, 2022, kwa siku kadhaa za shughuli za kiroho, kijamii, kimwili, na kiakili.
Kongamano la Vijana Waadventista wa Ulaya 2022 (AYC22), chini ya mada ya Plug In, lina lengo la  kuwasaidia vijana wa Kiadventista kuungana na Mungu na watu wanaowazunguka.
Viongozi wa vijana wa Divisheni za Kanisa la Wa Adventista wa Sabato barani Ulaya (EUD) na  (TED) wanasema wameongoza timu kupanga shughuli nyingi ambazo zinatoa fursa za mahusiano na ushirikiano wenye  matumaini yasiyokoma
“Tunaishi katika wakati ambao tuna nyaya nyingi za kuchaji vifaa katika nyumba yetu kuliko kitu kingine chochote unachoweza kufikiria. Daima tunahakikisha kuwa vifaa vyetu havikosi chaji,”"Mkurugenzi wa Vijana wa EUD Jonatan Tejel Tunahitaji kupeleka ukweli huu kwenye ulimwengu wa kiroho … ili kupata pumziko na mdundo wetu [na] kuungana na Mungu kikweli.”
AYC22 pia itajumuisha mashindano ya michezo mbalimbali ya utimamu wa  kimwili, uzoefu wa kipekee wa kitamaduni wa Kifini, na fursa za kuungana na kuwahudumia wengine
Waandaaji na washiriki wanatarajia kuwafikia na kuungana na wakazi 120,000 wa jiji lililoko mwendo wa saa moja kwa gari kaskazini mwa Helsinki, mji mkuu wa Finland.
Kongamano ambalo  hufanyika kila baada ya miaka minne, iliahirishwa mnamo mwaka 2021 kwa sababu ya vizuizi vya janga la Corona,lakini viongozi walisema wanafurahi wanaweza kukutana ana kwa ana  mwaka mmoja tu baadaye kuliko ilivyopangwa, mara ya mwisho kufanyika kwa kongamano hilo ilikuwa mwaka  2017 huko Valencia, Uhispania.

Kwa mujibu wa Tejel, karibu vijana wadogo na vijana wakubwa  wa Kiadventista wapatao  2,300 wamejiandikisha kwa kongamano la 2022 nchini Ufini, jambo ambalo limekuwa zaidi ya  makadirio ya waandaaji.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.