MTANGAZAJI

"UTATA'' KIFO CHA MWALIMU WA SHULE YA KANISA

Vyombo vya habari nchini India vinaripoti kwamba Jaishree Gilbert (64) aliyekuwa mwalimu katika Shule ya Sekondari ya Wa Adventista wa Sabato huko Lucknow, India, amefariki katika "mazingira ya kutatanisha" alipokuwa shuleni mnamo Julai 12, 2022.

Mkuu wa shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1915,Raj Durai Raj amesema Jaishree alifariki kwa kujiua na alikuwa amechanganyikiwa kiakili tangu kifo cha mumewe, Jaswant Gilbert, kutokana na mshtuko wa moyo mnamo Novemba 2021, limeripoti  The Times of India.

Mnamo Ijumaa, Julai 8, 2022, Jaishree Gilbert aliripotiwa kumpiga kiatu chake mfanyakazi ambaye alimshtaki kwa kumnyanyasa, amesema Durai Raj.

Ameeleza kuwa kamati ya uchunguzi iligundua madai yake hayana msingi,kwa hivyo, Jaishree Gilbert alisimamishwa kazi na kutakiwa kutoa cheti cha matibabu kinachothibitisha kuwa akili yake iko timamu kwa  kazi kabla ya kuanza tena majukumu yake shuleni hapo.

Durai Raj anasema Jumanne iliyofuata, Julai 12, 2022, Jaishree Gilbert alifika shuleni saa 1:25 asubuhi lakini hakuzungumza na mtu yeyote kisha Alikwenda moja kwa moja kwenye varanda ya ghorofa ya tatu ya shule na kuruka hadi kufa.

Wafanyakazi walitoka nje kwa kasi waliposikia kelele kubwa na kumkuta akiwa amelala kwenye dimbwi la damu. Walimkimbiza hospitalini ambako alitangazwa kuwa amefariki dunia.

Hata hivyo  Arvind Gilbert, mtoto wa Jaishree Gilbert anasema mama yake alikuwa na msongo wa mawazo baada ya kifo cha mumewe lakini alisimamishwa kazi kwa madai ya kipuuzi.

Kwa mujibu wa malalamiko yaliyowasilishwa Polisi na Naveen Singh Gilbert mtoto  mwingine wa Jaishree Gilbert, yanadai Mama yake alienda kukutana na mkuu wa shule mnamo Julai 12, 2022, kuomba kusimamishwa kwake kuondolewe. .

Baadaye, Naveen Gilbert alipokea simu na kutakiwa kwenda shule mara moja. Alipofika, anasema alimkuta mamake akiwa amelala kwenye gari la shule huku damu ikitoka kichwani na mdomoni, iliripoti News 18.

Naibu Kamishna wa Polisi Chiranjeev Nath Sinha anasema  Naveen Gilbert alitoa taarifa kwa polisi na kisha kumkimbiza mama yake katika hospitali ya kibinafsi, ambayo ilimpeleka hospitali nyingine, ambapo madaktari walitangaza kuwa amekufa baada ya kuwasili.

Mwenyekiti wa Umoja wa Ustawi wa Makanisa ya Wa Adventista ya India,K. R. Mathew, amedai katika barua pepe kwa vyombo vya habari kwamba alidai katika kwamba Jaishree Gilbert hakuambiwa ni kwa nini alikuwa akiombwa kutoa cheti cha matibabu cha "akili iliyo sawa kufanya kazi". 

"Alipoenda kwa mkuu wa shule mnamo Julai 12, 2022, kutafuta maelezo na kuendelea na kazi, Durai Raj alidaiwa kumsukuma nje ya ofisi na kusema kwamba anaweza kufukuzwa kazi. Akiwa amefedheheshwa na kushindwa na msongo wa mawazo na matusi, Jaishree Gilbert kisha akajiua"amesema Mathew. 

Mathew anadaiwa kuwa wasimamizi wa shule hawakuifahamisha polisi kuhusu kifo cha Jaishree Gilbert na wanaeneza habari za uwongo kimakusudi ili kuficha kilichotokea. Ambapo ameitaka Divisheni ya Kusini mwa Asia ya Kanisa la Wa Adventista wa Sabato kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo. 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.