MTANGAZAJI

MCHUNGAJI ASHINDA KESI YA KUKIUKA MASHARTI YA CORONA

 


Mahakama ya Canada  imetoa uamuzi unaomuunga mkono Mchungaji ambaye alipata umaarufu wa kimataifa kwa pingamizi lake dhidi ya vizuizi vya janga la Corona na ili kutaka uamuzi wa mahakama ya chini kumshikilia kwa kudharau maagizo ya kutofanya mikusanyiko.

Sarah Miller, wakili wa Mchungaji Artur Pawlowski ambaye anafahamika kwa kufanya mahubiri mitaani huko Calgary, Alberta, Canada, alitangaza katika ukurasa wake wa twitter Ijumaa kwamba Mahakama ya Rufaa ya Alberta ilimpa ushindi mchungaji huyo aliyezungumza waziwazi.

"Mahakama ya Rufaa ilifanya uamuzi kwa kauli moja, mzuri na kubatilisha matokeo ya dharau dhidi ya mteja wangu," Miller aliandika.

Uamuzi huo kwa kauli moja kutoka kwa jopo la majaji watatu uliondoa uamuzi wa mahakama ya chini unaowashikilia Pawlowski na kaka yake, Dawid, kwa kudharau mahakama kwa kufanya mkusanyiko usio halali wa hadhara kinyume na vizuizi vya mkoa wa Alberta kwa mikusanyiko mikubwa iliyowekwa wakati wa janga la Corona.

Mahakama iliamuru Kitengo cha Huduma za Afya cha Alberta kumlipa Pawlowski na kaka yake Dawid $15,733.59.

Video ya Pawlowski akikabiliana na maafisa wa afya ya umma wakiingia kanisani kwake kutaka kutekeleza vizuizi vya ibada wakati wa Corona ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari msimu wa joto wa mwaka 2021,ambapo majuma matatu baadaye video  nyingine ya Pawlowski akikabiliana na maafisa wa afya ya umma  nayo ilisambaa.

Muda mfupi baada ya video hizo zilizoonesha mabishano  makali kati ya Pawlowski na maafisa wa Afya kuhusu kutekeleza kuzuizi cha kukusanyika  kusambaa, Pawlowski na Kaka yake walikamatwa kwa kufanya ibada isiyo halali ya mtu binafsi ambayo ilikiuka vizuizi vya Corona.No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.