MTANGAZAJI

ALIYEFYATUA RISASI UWANJA WA NDEGE WA DALLAS ASHTAKIWA

 

 Mwanamke anayedaiwa kufyatua risasi kadhaa ndani ya uwanja wa ndege wa Dallas Texas  anakabiliwa na shtaka la kumpiga mtumishi wa umma kwa sababu alidaiwa kufyatua risasi moja kuelekea afisa wa polisi.
Afisa huyo wa Polisi alimpiga risasi na kumjeruhi Portia Odufuwa mwenye umri wa miaka 37 ambaye alipelekwa hospitali baada ya kupigwa risasi Jumatatu katika Uwanja wa Ndege wa Dallas Love Field.
Mkuu wa polisi wa Dallas Eddie Garcia alisema katika mkutano na waandishi wa habari Jumanne kwamba Odufuwa, ambaye amepigwa marufuku kumiliki bunduki, anaweza kukabiliwa na mashtaka ya ziada.
Hati ya mashiaka inaeleza kuwa Odufuwa, ambaye hakuwa na mizigo,aliingia eneo la kukatia tiketi, kisha akaingia kwenye choo, akiwa ameweka mikono mfukoni kwenye nguo iliyofuika kichwa,Garcia alisema kwamba kisha aliingia katika eneo la kukatia tiketi na kusema ana tangazo la kupiga risasi.
Video  za uchunguzi zilizotolewa na polisi zinaonyesha watu wakikimbia na kugonga maduka , wakianguka chini na kukimbia huku Odufuwa akianza kufyatua risasi.
Mamlaka bado inachunguza chanzo cha tukio hilo, inagwa Odufuwa amekamatwa mara kadhaa katika miaka ya hivi karibuni na ameonekana kuwa na kumbukumbu kushtakiwa zaidi ya mara moja.
Mwaka  jana Hakimu alimkuta mwanamke huyo  hana uwezo wa kujibu mashtaka baada ya kushtakiwa kwa kutoa ripoti ya uwongo, rekodi za mahakama zinaonyesha. Hakimu aligundua kuwa hakuwa hatari kwa wengine na kumpeleka kwa huduma za afya ya akili kwa wagonjwa wa nje.
 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.