MTANGAZAJI

WASIFU WA KIONGOZI WA WA ADVENTISTA ULIMWENGUNI MCH TED N.C WILSON

 


 

Kamati kuu ya Utendaji ya Kanisa la Wa Adventista wa Sabato ulimwenguni imepiga kura ya kumchagua tena Mchungaji Ted  Wilson kuwa kiongozi wa Kanisa hilo ulimwenguni kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.


Kamati ya Utendaji iliyokutana huko St. Louis, Missouri Marekani kwenye Mkutano wa 61 wa Konferensi Kuu ya Kanisa la Wa Adventista wa Sabato Duniani uliofanyika mwaka huu baada ya kuahirishwa mara mbili kutokana na janga la Uviko 19.


Wilson ambaye utakuwa ni muhula wake wa tatu sasa kuongoza kanisa hilo, alichaguliwa kuwa kiongozi wa Kanisa la Wa Adventista wa Sabato Ulimwenguni kwa mara ya kwanza katika Kikao cha Konferensi Kuu ya 2010, akichukua nafasi ya Jan Paulsen, ambaye alihudumu katika nafasi hiyo  tangu 1999. Mnamo mwaka 2015, katika Kikao cha 60 cha Mkutano Mkuu, Wilson alichaguliwa tena kwa muhula wa pili wa miaka mitano.


Ted N.C. Wilson  anayezungumza Kiingereza,Kifaransa na Kirusi ni Mtoto wa aliyekuwa Kiongozi wa Kanisa la Wa Adventista wa Sabato Ulimwenguni Neal C.Wilson 1979 hadi 1990,  amehudumu katika  Kanisa la Wa Adventista  wa Sabato kwa  majukumu mbalimbali kwa  miaka 50. Alianza akiwa  mchungaji katika Konferensi ya The Greater New York mnamo 1974, na baadaye akahamia katika majukumu ya kiutawala na huduma za kigeni.


Amewahi kuwa Kiongozi wa Kanisa la Wa Adventista wa Sabato katika Divisheni ya Trans Euro Asia makao yake makuu yakiwa Moscow Urusi mwaka 1992 hadi 1996,kabla ya hapo akifanya kazi katika Divisheni ya Afrika na Bahari ya Hindi huko Abidjan Ivory Coast hadi mwaka 1990 ambapo alikuwa Mkurugenzi wa Idara na Katibu Mtendaji.Amewahi pia kuwa Mkurugenzi na baadaye Katibu Mtendaji kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Kanisa la Wa Adventista wa Sabato zilizopo Silver Spring Maryland Marekani.


Wilson ana shahada ya Udaktari wa Falsafa katika Elimu ya Dini kutoka Chuo Kikuu cha New York,Shahada ya Uzamili ya elimu ya Uungu kutoka Chuo Kikuu cha Andrews, na Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Afya ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Loma Linda.

Akiwa Loma Linda  alikutana na mke wake, Nancy, mtaalamu wa tiba ya viungo, na kwa pamoja wamefanikiwa kupata watoto  watatu, Emilie, Elizabeth, na Catherine.



No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.