MTANGAZAJI

WAMISHONARI 17 WATEKWA HAITI

 

Wamishonari  17 kutoka Marekani na Canada ambao miongoni mwao ni vijana chini ya miaka 18 wametekwa nchini Haiti mwishoni mwa juma kwa mujibu wa taasisi ya Umoja wa Huduma ya Misaada ya  Kikristo  (OCAM).
 
Taarifa ya OCAM iliyotolewa Ohio Marekani  Jumapili imeonesha kuwa waliotekwa ni Raia 16 toka Marekani na Canada mmoja,"tunatafuta mwongozo wa suruhisho  kutoka kwa MUNGU na mamlaka zinatafuta njia ya kusaidia"Ilieleza taarifa hiyo.
 
CNN imeripoti kuwa kundi hatari la uhalifu nchini Haiti linaaminika kuhusika na utekaji huo kwa mujibu wa duru za mamlaka za usalama za nchi hiyo.
 
Mamlaka hiyo inaamini kuwa kundi hilo liitwalo  "400 Mawozo" liliwateka wamishonari hao baada ya kutembelea kituo cha kuwatunza yatima Jumamosi Croix des Bouquets kaskazini mashariki mwa Mji Mkuu wa Haiti,  Port-au-Prince.
 
 Walipokuwa wakisafiri kutoka kituo hicho kuelekea Titanyen, kaskazini mwa Port-au-Prince,wanachama wa 400 Mawozo  wakiwa na siraha walilisimamisha gari.
 
 Mmoja wa waliotekwa alituma ujumbe wa kuomba msaada kwenye jukwaa la Whatsapp wakati tukio hilo linatokea.
 
 Kundi la  400 Mawozo limekuwa likijiimarisha katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ambapo kwa sasa linaidadi ya watu 150 na likishika hatamu katika eneo la Croix des Bouquets, kwa mujibu wa vyombo vya Usalama  vya Haiti.
 
 Kwa mujibu wa taarifa za Kituo cha Utafiti na Uchambuzi wa Haki za Binadamu nchini Haiti (CARCH) takribani matukio 628  ya utekaji 628 yametokea kuanzia Januari, yakihusisha wageni 29,. Kundi la The 400 Mawozo limedai fidia ya karibu Dola za Kimarekani 20,000. 
 
 Haiti imekuwa katika hali tete ya usalama toka kuuawa kwa alyekuwa Rais wa nchi hiyo Jovenel Moïse mwezi Julai,huku ikikumbwa na tetemeko la ardhi Agosti mwaka huu ambapo  watu 2,200 walipoteza maisha. 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.