MTANGAZAJI

BARAKOA YAZUIA NDEGE KUONDOKA UWANJANI

 

Abiria (Jina lake halikuwekwa wazi) ambaye aligoma kuvaa Barakoa akiwa ndani ya ndege ya Abiria ya  Shirika la Ndege la American  Airlines amesababisha Ndege ya namba AA 2438 iliyokuwa ikisafiri Oktoba 15,2021 kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa George Bush jijini Houston Texas kuelekea Dallas kuchelewa kuondoka kwa zaidi ya nusu saa jambo lililosababisha usumbufu kwa abiria wengine hasa waliokuwa wakiwahi kuunganisha Ndege kwenda majimbo mengine nchini humo.

Kuanzia Februari mwaka huu,Mamlaka nchini Marekani inawataka abiria wote wanaotumia usafiri wa Anga  nchini Marekani kuvaa Barakoa muda wote wanapokuwa kwenye viwanja vya Ndege na wanapokuwa safarini ndani ya Ndege ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na janga la Corona.
 
Hivi karibuni Rais wa Marekani Joe Baiden aliigiza Mamlaka inayosimamia Usalama katika  Sekta ya Usafirishaji kuongeza kiasi cha tozo ya faini kwa abiria wanaokaidi kuvaa Barakoa iwe kuanzia Dola za Kimarekani  500 hadi  1000 kwa anayekaidi mara ya kwanza na akibainika amerudia kosa hilo alipe faini ya Dola 1000 hadi Dola 3,000. 
 
Wafanyakazi wa Ndege hiyo ambayo awali ilipaswa kuondoka Houston saa 1:30 jioni waliwatangazia abiria waliokuwa kwenye Ndege hiyo kushuka ili Abiria aliyekataa kuvaa Barakoa aweze kuchukuliwa na askari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houston ambapo walifanya hivyo na Ndege hiyo iliondoka saa 2:08 usiku na kufika Dallas saa 9:21usiku  tofauti na muda wa awali ambao ulikuwa ni saa 8:59 usiku.
 
Taarifa ya Rubani wa Ndege kwa abiria ikiwemo kuomba radhi kabla ya kuondoka kutokana na mkasa huo ilieleza kuwa huenda abiria aliyegoma kuvaa Barakoa akasafiri Jumanne ya juma lijalo na suala hilo sasa liko kwa mamlaka za usalama katika uwanja huo.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.