WATEKAJI WATAKA DOLA MILIONI MOJA KWA KILA KICHWA
Kikundi cha Wahalifu huko Haiti kimeeleza kuwa kinataka malipo ya Dola milioni moja kwa kila mtu ili kuwaachia Wamishonari na watoto lililowateka.
Waziri wa Sheria Liszt Quitel amethibitisha kwamba matakwa hayo yamepokelewa iikiwa ni masharti ya kuachiwa kwa watu hao 17 waliotekwa nchini Haiti.
Wamishonari 17 kutoka Marekani na Canada ambao miongoni mwao ni vijana chini ya miaka 18 walitekwa nchini Haiti asubuhi ya Oktoba 16 mwaka huu.
Kundi hatari la uhalifu nchini Haiti 400 Mawozo linaaminika
kuhusika na utekaji huo kwa mujibu wa duru za mamlaka za usalama za nchi
hiyo.
Taarifa ya Mkuu wa Idara ya Habari ya Ikulu ya Marekani Jen Psaki amesema kuwa Ikulu hiyo na FBI wanafanya jitihada za kuwaokoa mateka hao.
Kwa
mujibu wa taarifa za Kituo cha Utafiti na Uchambuzi wa Haki za Binadamu
nchini Haiti (CARCH) takribani matukio 628 ya utekaji 628 yametokea
kuanzia Januari, yakihusisha wageni 29,Kundi la 400 Mawozo
limedai fidia ya karibu Dola za Kimarekani 20,000.
Post a Comment