MTANGAZAJI

FAMILIA ZATANGAZA KUWASAMEHE WATEKAJI

 

 Familia za wamishonari 17 waliotekwa huko Haiti zimesemea zimewasamehe wanachama wa kundi lililohusika na tukio hilo ambalo mpaka sasa linadai fidia ili kuwaachia huru.

Ujumbe wa familia hizo umewasilishwa kupitia Shirika la  Kikristo linalojihusisha na misaada la nchini Marekani ambalo lilikuwa linaratibu ziara ya wamishonari hao nchini Haiti. 
 
Utekaji huo ulitokea Oktoba 16,2021 ambapo walikuwa wakisafiri kuelekea uwanja wa Ndege baada ya kutembelea kituo cha watoto yatima kilichopo karibu na Mji Mkuu Port-au-Prince.
 
 Waliotekwa ni watoto watano ambapo mmoja kati yao ana miezi sita,Watu wazima 16 kutoka Marekani na mmoja toka Canada.
 
Kundi la  400 Mowozo ambalo linaelezwa kuhusika na utekaji huo limetangaza kutaka fidia ya Dola milioni 1 za Marekani kwa kila kichwa na mmoja wa kiongozi wake  Wilson Joseph ametoa vitisho vya kufanya mauaji ikiwa fidia hiyo haitatolewa.
 
 CAM imeeleza kuwa kumekuwepo na vilio na maombi vya  maelfu ya watu kufuatia kinachoendelea na imesisitizwa watu kuendelea kuomba.

Ingawa kumekuwa na vitisho kwa wapendwa wao,Baba wa mateka wawili wametuma ujumbe wa kuwasamehe watekaji.
 
Familia nyingine imesema "Kama familia tunatoa msamaha kwa watu hawa na hatuna kinyongo nao"

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.