MTANGAZAJI

WAKAMATWA KWA KUTELEKEZA MAITI NA WATOTO MWAKA MZIMA

 

Mwanamke mmoja na mpenzi wake wamekamatwa Oktoba 26,2021 kutokana na kifo cha mtoto wa mwanamke huyo, ambapo mabaki ya mwili wa marehemu yamekutwa ndani ya nyumba aliyopanga,pamoja na ndugu watatu waliosalia ambao inaonekana wametelekezwa.

 Taarifa ya Afisa wa Polisi wa Harris,Houston kupitia twitter Ed Gonzalez imeeleza kuwa Bryan W. Coulter (32)  ameshitakiwa kwa mauaji jumanne hii,Mama wa Marehemu Gloria Y. Williams (36)  ameshtakiwa kwa kosa la jinai la mauaji ya kujeruhi mtoto,kushindwa kupata matibabu,na kushindwa kutoa uangalizi sahihi kwa mtoto.

  Mmoja wa watoto waliotelekezwa mwenye miaka 15 alitoa taarifa Polisi Jumapili ya Oktoba 24,2021 na kueleza kuwa ni mwaka mmoja sasa  tangu mdogo  wake  mwenye miaka 9 afariki dunia na mwili wake uko ndani.

Watuhumiwa Wote wamepelekwa gereza la Harris bila dhamana,haijafahamika kama watuhumiwa hao wanamwanasheria,Huenda wakasomewa mashitaka zaidi amesema Gonzalez.

Taasisi ya Sayansi ya Uchunguzi wa matukio ya mauaji ya Houston imetoa taarifa ya awali kuwa chanzo cha kifo cha mtoto huyo kutokana na vurugu zilizosababisha majeraha mengi yaliyotokana na matumizi ya nguvu.

 Michele Arnold msemaji wa Taasisi hiyo amesema kituo hicho hakikuweza kutoa taarifa zaidi.

 Naibu msemaji wa Ofisi ya Polisi ya Harris Thomas Gilliland,  amesema hawezi kutoa taarifa zaidi kwa sababu bado mamlaka zinaendelea na uchunguzi wa kifo hicho.

Maafisa walikuta kijana huyo na ndugu zake wengine mmoja wa miaka 10 na mwingine miaka 7 walikuwa wakiishi peke yao katika nyumba hiyo,Ambao aliwaeleza kuwa wazazi wao hawaishi hapo kwa miezi kadhaa sasa.

Kwa mujibu wa Gonzalez watoto hao walikuwa wakijitafutia mahitaji ikiwemo chakula ambapo Mkubwa ndiye aliyekuwa akiwatunza wadogo zake wawili.

Walipokuwa wakiishi hakukuwa na umeme,ambapo majirani walikuwa wakiwasaidia kuchaji simu na kuwanunulia chakula.

Watoto hao watatu walionekana dhaifu walichuliwa na kupelekwa hospitali kwa ajili ya chunguzi na matibabu.

 


.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.