MTANGAZAJI

ASHITAKIWA KWA MAUAJI YA MTOTO WA MPENZI WAKE

 

 


Mwanamme mmoja amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya  tuhuma za mauaji ya mtoto wa kiume mwenye miaka minane wa  Mpenzi wake.

Brian W. Coulter (31) amesomewa mashtaka ya mauaji ya mtoto ambaye mabaki ya mwili wake yalikutwa nyumbani alikotelekezwa baada ya kuuawa kwa karibu mwaka mzima jijini Houston,Marekani.  Mkuu wa Polisi wa Manispaa ya Harris amesema.Alhamisi ilikuwa ni mara ya kwanza kusomewa mashitaka kabla ya hukumu.

Coulter amesaini fomu maalum ya mahakama ambayo inamtaka kutofanya mawasiliano yoyote na watoto watatu waliobaki,Sehemu ya Maelezo ya  dhamana yake yenye kiasi cha Dola Milioni moja za Marekani  iwapo atatoa kiasi hicho itamtaka kuwekewa kifaa maalum mguuni ili kufahamu alipo,asitoke nyumbani na asifanye mawasiliano Gloria Williams mpenzi wake na Mama wa Watoto.

Gloria Williams ameshtakiwa kwa tuhuma za kumwumiza mtoto na kuficha ushahidi,japo alitakiwa kuwepo mahakamani Ijumaa hii na sasa atapangiwa siku nyingine juma lijalo.

Kwa mujibu wa mahakama Brian Coulter, alimpiga mtoto huyo mbele ya wadogo zake ambao wamesema alimchapa usoni,mibuuni,kwenye makalio na mgongoni na aliendelea kumpiga mateka wakati akiwa ameshinda kutembea.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.