SILAHA YAUA MTOTO AKIICHEZEA NA MWENZAKE
Mtoto wa miaka 10 amefariki dunia baada ya ajali ya kupigwa risasi Kaskazini mwa Houston,Polisi wamesema.
Mauaji yametokea Mtaa wa Willow Place saa sita mchana Oktoba 28,2021.
Polisi wameeleza kuwa Mama wa Mtoto huyo wa kiume alimtuma yeye na mtoto mwingine ambaye ni binamu yake mwenye miaka 11 kwenda kuchukua kitu kwenye gari alilokuwa ameegesha ndipo mtoto huyo alipoiona bastola ndani ya gari.
Watoto hao walianza kucheza na silaha hiyo na ndipo ilipofwatuka na risasi kumpiga mtoto mwenye miaka 10,utapelelezi haujabaini ni mtoto yupi alikuwa ameishika bastola hiyo wakati inafwatuka .
Baada ya tukio hilo mtoto wa miaka 10 alipelekwa kwa Hospitali ya karibu na baadaye akafariki.
Polisi imesema bado inaendelea na uchuguzi kuhusu tukio hilo.
Post a Comment