MTANGAZAJI

KADI BANDIA ZAIDI YA 3000 ZA CHANJO YA COVID-19 ZAKAMATWA

 
 Wakala wa Mamlaka ya  Forodha na Ulinzi wa Mipaka nchini Marekani (CBP) imekamata kadi zingine bandia za chanjo ya Covid-19 katika jiji la Memphis ikiwa ni mwendeleo wa matukio ya ukamataji wa maelfu ya kadi bandia  katika jiji hilo kwa mwaka huu. 
 
 Taarifa ya CBP hiyo imeeleza kuwa maafisa wake huko Memphis waligundua kifurushi waichokitilia shaka kilitumwa kutoka Shenzhen, China, kwenda jimbo la New Orleans,kilichokuwa kimeandikwa "PAPER CARD, PAPER" ambapo waligundua kilikuwa na kadi 15 bandia  za chanjo ya Covid-19.
 
Hii si mara ya kwanza kupatikana kwa kadi bandia katika jiji hilo,Wakala wa Mamlaka ya Forodha na ulinzi wa Mipaka jijini Memphis imekamata vifurushi 121 vilivyokuwa na kadi bandia za chanjo  3,017 mwaka huu.
 
Shule na Vyuo Vikuu nchini Marekani vimeanza kuwataka wanafunzi kuonesha uthibitisho wa kuchanjwa chanjo ya Covid-19,ingawa baadhi ya maofisa wa CBP wana wasiwasi huenda wanafunzi wakaonesha vitambulisho bandia,ingawa baadhi ya shule zimeeleza kuwa kuonesha taarifa za uongo katika zoezi hilo kutasababisha mhusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
 
Hata hivyo taarifa za watu wanaochanjwa zote ikiwemo jina,anuani za makazi,namba ya kitambulisho cha mkaazi,tarehe ya kuzaliwa,kituo ulipochanjwa,aina ya chanjo,siku ya chanjo,zimekuwa zikichukuliwa na kuhifadhiwa katika kanzidata za vituo na hospitali zinazotoa chanjo jambo ambalo ni rahisi kufahamika kwa mtu ambaye amechanjwa na ambaye hajachanjwa.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.