MALIPO YA MAOMBI YA BIASHARA TANZANIA KWA NJIA YA MTANDAO
Serikali nchini Tanzania iko mbioni kunzisha mpango wa malipo ya maombi ya biashara kwa njia ya mtandao.
Mpango huo umetangazwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya maafisa Biashara kutoka mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida, jijini Dodoma.
Nyaisa amesema kuwa hivi sasa maombi yote ya leseni yatakuwa kwenye mfumo mmoja ambapo mfanyabiashara atakuwa anaomba leseni kupitia kwenye mtandao na kulipia kwa kutumia namba maalumu ya malipo serikalini (Control Number) na kwamba mpango huo utapunguza kwa asilimia kubwa ubadhirifu hivyo kuongeza wigo wa mapato.
Amewaonya waliokuwa na tabia hiyo ya ubadhilifu kuachana nayo na kinachotakiwa ni kujipanga upya kuchapa kazi ya kuhakikisha katika maeneo yao wanaongeza wigo wa kurasimisha wafanyabiashara ili serikali iwe inaongeza mapato.
"Inatakiwa Afisa Biashara atengeneze Kanzi Data (Database) ya idadi ya wafanyabiashara waliopo katika eneo lake itasaidia sana kurahisisha utendaji kazi. Msikurupuke sana kufunga biashara, hivi ukifunga wewe unategemea nini, hujui unachangia kuuaq uchumi wa nchi?" Alihoji Nyaisa.
"Serikali ina shida na mfanyabiashara na mfanyabiashara ana shida hivyo msikurupuke kuwafungia biashara, kaeni muelewane, mtumie busara lakini pia mkae mkijuwa kuwa licha ya Serikali kutaka mapato lakini kazi yake kubwa ni kutoa huduma," amesema Nyaisa.
Amewataka maafisa biashara kuwajengea mazingira mazuri wawekezaji wanaokwenda katika maeneo yao, badala ya kuwatendea mambo yasiyofaa yanayowakatisha tamaa ikiwemo kuwaomba rushwa.
Post a Comment