MAUAJI YA KUTUMIA SILAHA YATIKISA MAJIJI MAREKANI MWISHONI MWA JUMA
Eneo la Colorado Springs limeshuhudia majibizano ya kutupiana risasi kwa bunduki ijumaa iliyopita ambapo watu watano wamejeruhiwa,usiku wa ijumaa.
Katika jimbo la Louisiana, watu sita walipigwa risasi na wawili kupoteza maisha mapema asubuhi siku ya jumamosi.
Huko Flint, Michigani, mwanamke amefariki kutokana na kupigwa risasi na polisi baada ya majibizano ya risasi kati ya Polisi na mwanamke huyo.
Mshukiwa ambaye jina lake halikutajwa alifariki hospitalini kutokana na tukio hilo,Polisi katika Jimbo la Michigani imeeleza katika taarifa.
Vyombo vya Habari huko Chicago vimeripoti takribani watu watano wameuawa na wengine 44 kuumia kutokana na mashambulizi ya bunduki katika eneo hilo mwishoni mwa juma.
Katika mji wa Wichita,Kansas Afisa wa Polisi alikimbizwa hospitalini akiwa na hali mbaya baada ya kupigwa risasi kwa mujibu wa Afisa wa Polisi Gordon Ramsay na mtuhumiwa katika tukio hilo aliuawa kwa kupigwa risasi.
Huko Texas,watoto wawili walikuwa miongoni mwa watu wanane waliopigwa risasi kwenye sherehe katika eneo la Old East Dallas.Polisi wamesema mashambulizi ya risasi yalitokea baada ya mabishano yaliyosababisha kutokuelewana kwa wahusika wa sherehe hiyo.
Kaskazini mwa California,watu saba walipigwa risasi na mmoja kufariki karibu na Ziwa Merritt katika jiji la Oakland.Kwa mujibu wa Kitengo cha Polisi cha Oakland tukio hilo limetokea wakati maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika karibu na ziwa hilo ambapo Polisi walikuwepo kuhakikisha usalama wa raia.
Post a Comment