MTANGAZAJI

MITAZAMO YASABABISHA MGAWANYIKO MIONGONI MWA WAKRISTO MAREKANI

 

Ripoti ya Mtandao wa US Today imeeleza kuwa bado kuna mgawanyiko  miongoni mwa Wakristo nchini Marekani kulikosababishwa na uchaguzi wa mwaka 2020, masuala ya ubaguzi,na uvaaji wa Barakoa.

 Kwa mujibu wa Kituo cha Mafunzo ya Ukristo Duniani kuna zaidi ya madhehebu ya Kikristo 200 nchini Marekani huku ikielezwa kuwa kuna mijadala inayoendelea ya kugawanyika kwa miongoni mwa madhehebu hayo katika miaka ya hivi kribuni.

Migawanyiko hiyo inasababisha kutelekezwa kwa  makanisa,Mwaka jana Mtandao wa Barna ambao huandika tafiti kuhusu masuala yanayohusu Ukristo uligundua kuwa takwimu za ukristo zimeshuka karibu nusu toka mwaka 2000.Huku mtandao wa Gallup ukitoa taarifa hivi karibuni kuwa takwimu za ushirika wa waumini katika makanisa nchini Marekani umeshuka chini ya  asilimia 50 katika miongo minane iliyopita.

Takwimu za mwaka 2018/19 zinaonesha kuwa asilimia 65 ya watu wazima nchini Marekani walijitambulisha kuwa ni Wakristo,asilimia 75 mwaka 2015,Asilimia 70.6 mwaka 2014,Asilimia 78 mwaka 2012,wakati mwaka 2001 ilikuwa asilimia 81.6 na asilimia 85 kwa mwaka 1990.

 Utafiti uliofanywa mwaka 2017 na kituo cha utafiti cha LifeWay ulionesha kuwa asilimia 66 ya wamarekani wenye umri kati ya miaka 23-30 walisema wameacha kwenda kanisani kama iliyokuwa kawaida yao baada ya kufikisha miaka 18. Na miongoni mwa sababu kubwa ni kuona kuwa baadhi ya waumini wamegawanyika,wanahukumu au wanafiki.

 Mchungaji Andy Stanley toka Atlanta hivi karibuni alieleza sababu tano zinazosababisha mtu kuacha kanisa,Moja ya sababu ni uzoefu mbaya alioupitia wakati akiwa kanisani ambapo baadhi ya washiriki  huona kuwa wao ni bora kuliko wengine.



No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.