MTANGAZAJI

TCRA YATAKIWA KUONGEZA KASI YA UTOAJI WA ELIMU KWA UMMA

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini Tanzana Dkt. Faustine Ndugulile ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha kwa umma kuhusu matumizi ya mtandao kwa kuwa mpaka sasa kiwango cha kuelimisha umma kinachotolewa na Mamlaka hiyo hakitoshelezi.

 Dkt. Ndugulile ametoa agizo hilo alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo Zanzibar Machi 11,mwaka huu akiambatana na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rahma Kassim Ali, Makatibu Wakuu wa Wizara yake Dkt. Zainab Chaula na wa Zanzibar Amour Bakari pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara hizo.


“TCRA bado sijaridhishwa na kiwango cha elimu ya matumizi ya mtandao mnayoitoa kwa ummavna katika utoaji wa elimu kwa umma mkumbuke kuelimisha jamii kuhusu wajibu na haki zao ili wanapopata shida mitandaoni wajue wapite katika njia zipi”, Dkt. Ndugulile.

 Dkt Ndugulile ametoa maelekezo kwa TCRA kuimarisha mfumo wa ukaguzi wa vifaa vya kielektroniki vinavyouzwa na wafanyabiashara ili kuthibitisha ubora na uhalali wa vifaa hivyo ikiwezekana viwekewe alama kuwa vimekaguliwa ili kuhakikisha usalama wa vifaa hivyo kwa matumizi ya wananchi.


Katika hatua nyingine Dkt. Ndugulile ameielekeza TCRA kuhakikisha Shirika la Posta Tanzania linafanya kazi yake ya kusafirisha vipeto na vifurushi kwa kufuata sheria ya EPOCA inayosema kuanzia uzito wa 0 hadi 0.5 gms haruhusiwi msafirishaji yeyote kusafirisha isipokuwa Shirika hilo na kuitaka TCRA kusimamia vema suala hilo.


Waziri huyo  Mamlaka hiyo kwa kupeleka vifaa vya TEHAMA katika
shule ya Sekondari ya wasichani ya Utaani iliyopo Wete Zanzibar kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi na walimu wa shule hiyo, vifaa hivyo ni pamoja na kompyuta 10, printa, projekta pamoja na kuunganisha huduma ya mtandao katika shule hiyo toka mwaka 2016 na mpaka sasa
bado vipo na vinaendelea kutumika.


Naye Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe.Rahma Ali ameitaka TCRA kuendelea  na utaratibu wa kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi sahihi ya TEHAMA huku wakijikita zaidi kwenye matumizi ya simu za mkononi.


Kwa upande wa Mkuu wa TCRA wa ofisi ya Zanzibar Esuvatie Masinga amesema kuwa Mamlaka hiyo inaendelea kujipanga vizuri katika utoaji wa elimu kwa umma na wiki hii tayari wameshatoa mafunzo ya matumizi ya TEHAMA kwa masheha 120 kwa Unguja na Pemba.No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.