MTANGAZAJI

RUBANI KIKE MWAFRIKA WA KWANZA NCHINI AFRIKA KUSINI



Mwanamke wa kwanza  Rubani wa helikopta mwafrika  Refilwe Ledwaba  ana maneno ya ushauri kwa yeyote ambaye anaogopa kubaguliwa na kumfanya kutotimiza  ndoto zake maishani.

 Badala ya kuwaangalia wale wanaokusudia kukurudisha nyuma,tafuta wengi wa watu ambao watafurahi kuona unachokifanya na ungana nao katika kutimiza malengo.

Akiwa amekulia katika mazingira ya ubaguzi huko Afrika ya Kusini akiwa na  ndugu zake 6 na kulelewa na Mama peke yake, Ledwaba alikuwa karibu sana na jamii na hakuwa na taarifa sahihi za jamii zingine duniani .

 Ilikuwa wakati akipata mafunzo ya kuwa mhudumu wa ndege ndipo alipoanza kupenda kuwa msaidizi wa rubani,Rafiki yake wa kike mzungu alimtia moyo kujifunza urubani na akampa ahadi ya kumfundisha bure iwapo angechangia gharama za mafuta.

Mwaka 2005 alipata nafasi ya kujifunza kuendesha helikopta katika shule ya serikali nje ya jiji la Durban,ambako aliweka juhudu na maarifa kuhakikisha anafanya vyema.

Kwa mara nyingine tena mwanamme wa mzungu alimtia shime na kumwambia asikate tamaa anasema.Na muda wa kuendesha helikopa akiwa peke yake kwake aliona ilikuwa ni kuondoa kizingiti cha jinsia na ubaguzi wa rangi.

Miezi michache baadaye ndipo akafanikiwa kumaliza mafunzo hayo na  kuwa mwanamke wa kwanza rubani wa helikopta kujiunga na Jeshi la Polisi nchini Afrika ya Kusini. 

 Kwa sasa ni Mkufunzi wa Urubani anayetambuliwa na Serikali,akiwa na Taasis yake binafsi inayojihusisha na mafunzo ya Urubani kwa wasichana Barani Afrika  (GFPA) ), ambapo kwa zaidi ya karne ametoa mafunzo ya Urubani kwa mamia ya vijana wa kike ikiwa inafanya kazi katika nchi nne barani Afrika.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.