MTANGAZAJI

UTAFUNGUA IPHONE UKIWA UMEVAA BARAKOA

Baada ya takribani mwaka mmoja sasa wa matumizi ya Barakoa Duniani katika kujikinga na janga la Corona.Kampuni ya Apple inafanya mchakato wa kuwezesha watumiaji wa iphone kuzifungua simu hizo kwa kutumia teknolojia yake ya utambuzi wa sura (Face ID) wakiwa wamevaa Barakoa jambo ambalo awali halikuwepo.

Japo teknolojia hiyo haijakamilika tayari ni sehemu ya mkakati wa wataalamu wa mifumo wa Kampuni hiyo katika toleo la program endeshi iOS 14.5 litakapotoka,toleo lililopo kwa sasa ni iOS 14.4

 Mtandao wa Engadget unaofanya uchambuzi wa Teknolojia mbalimbali umeeleza kuwa teknolojia hiyo itakubali kufanyakazi kwa iphone kama mtumiaji atakuwa ana saa ya Apple (Apple Watch)

Ikiwa saa yako haijafungwa,mtumiaji utaelekeza sura yako kwa Iphone ukiwa na Barakoa na simu itafunguka ambapo saa ya Apple itakujulisha kila unapofungua simu yako.

Teknolojia hii imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu,Aprili mwaka jana Apple walitoa taarifa ya sababu za Utambuzi wa Sura (Face ID) kutofanya kazi kwa mtu aliyevaa Barakoa.

Face ID ni teknolojia ya simu za iphone inayofanya kazi kwa kutambua macho,pua,na mdogo vikiwa vinaonekana,Ingawa msemaji wa Apple ameeleza kuwa watumiaji wa simu hizo wataendelea na utaratibu wa awali wa kuweka namba za siri wakiwa wamevaa Barakoa.

 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.