MTANGAZAJI

MCHUNGAJI WA WAADVENTISTA NA BINTI YAKE WALIOKUWA WAMETEKWA WAPATIKANA


Mchungaji Elie Henry,Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika Divisheni ya Inter America pamoja na binti yake Irma wamepatikana wakiwa salama baada ya kuachiwa na watekaji Disemba 28,mwaka huu huko Port au Prince,Haiti,Mchungaji Henry na Irma waliripotiwa kutekwa jioni ya Disemba 24 mwaka huu.

Taarifa ya kupatikana kwa Mchungaji huyo na binti yake ambao hawakuonekana kwa muda wa siku nne kwa kile kilichoripotiwa na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa walitekwa imetolewa Disemba 28,2020  kupitia tovuti ya Divisheni ya  Inter America.

 "Nimezungumza na Mch Henry na amenifahamisha kwamba yeye na Irma waliungana na familia huko Katlie mjini Port au Prince na wako salama"Amesema Mch Leonard Johnson,Katibu Mkuu wa Divisheni ya Inter America

“Tunamshukuru MUNGU kwa kuwalinda,Viongozi wa Divisheni yetu na waumini wa Kanisa la Waadventista Ulimwenguni waliomba ili waachiwe hivyo tunamshukuru MUNGU" amesema Mch Johnson.

Kwa niaba ya Uongozi wa Divisheni hiyo Mchungaji Johnsona ametoa shukrani kwa watu binafsi,taasisi,waliofanyakazi bila kuchoka na waliioomba kuhakikisha Mchungaji Henry na Irma wanapatikana wakiwa salama.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.