MTANGAZAJI

MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA DODOMA


Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt Ibenzi Ernest akimuongoza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe (aliyevaa kaunda suti) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, Dk. Doroth Gwajima  (wa tatu kulia) kwenda kuzindua ukarabati wa chumba cha dharula na uangalizi wa wagonjwa mahututi  (ICU),  wakati wa maadfhimisho ya miaka 100 tangu Hospitali hiyo hiyo ianzishwe 1920. Picha zote na Richard Mwaikenda

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe  (wa pili kushoto ) akikata utepe kuzindua rasmi ukarabati wa chumba cha dharula na uangalizi wa wagonjwa mahututi (ICU), katika Hospitali hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, Dkt. Doroth Gwajima. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe akikagua chumba cha uangalizi wa wagonjwa mahututi (ICU).


Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ibenzi Ernest akimuongoza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe kukagua wodi ya wanawake ambayo imekarabatiwa na kuwekwa vifaa vipya ikiwemo vitanda, magodoro na vinginevyo.



Jengo la Wazazi
Jengo la Bima ya Afya

Wanafunzi wa Chuo cha Afya Mirembe, mkoani Dodoma wakitumbuiza kwa wimbo maalumu wakati wa maadhimisho hayo.




Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, Dk. Doroth Gwajima  akitoa neno  wakati wa maadhimisho hayo.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akitoa ahadi ya kujenga choo na bafu eneo la wananchi wanaosubiria wagonjwa wao katika Hospitali hiyo.



Aliyekuwa Muuguzi Mkuu wa Mkoa  Anatolia Mkindo akikabidhiwa cheti cha kutambua mchango wake katika hospitali hiyo kabla ya kustaafu.  Baadhi ya watumishi wa hospitali waliostaafu walitunukiwa vyeti.

Happy Mwaikugile ambaye ni mmoja wa wafanyakazi bora akilakiwa kwa furaha na wafanyakazi wenzie baada ya kutunukiwa tuzo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe (kulia) akimkabidhi tuzo maalumu Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ibenzi Ernest kwa uongozi wake thabiti.

 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.