MTANGAZAJI

MAKATIBU WAKUU SADC-TROIKA WAJADILI MASUALA YA SIASA,ULINZI NA USALAMA.

 


 

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akiwasilisha mada
katika Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC ya ushirikiano
katika siasa, ulinzi na Usalama unaondelea Mjini Gaborone, Botswana

Makatibu Wakuu wa SADC -TROIKA wamekutana na kujadiliana Mambo
mbalimbali yakiwemo masuala ya hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ndani
ya SADC mjini Gaborone, Botswana.


Awali, Mkutano wa Makatibu Wakuu ulifunguliwa na Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana,
Bw. Gaeimelwe Goitsemang ambae pia alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano
huo.


Ni mara ya kwanza kwa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika ( SADC) kukutana ana kwa ana tangu
ulipotokea ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (Covid-19).


Kwa upande wa Makatibu wakuu waliohudhuria katika Mkutano huo
kutoka Tanzania ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge,
pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt.
Faraji Mnyepe.


Mkutano wa Makatibu Wakuu ulifuatiwa na Mkutano wa Dharua wa
Baraza la Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano katika Siasa, Ulinzi
na Usalama baadae leo mchana mjini Gaborone.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.