MTANGAZAJI

MAPANGO YA AMBONI TANGA YAWEKEWA TAA KWA NDANI


Mamlaka  ya Hifadhi ya Ngorogoro imefanya maboresho ya miundo mbinu kwenye Mapango ya Amboni yaliyopo Jijini Tanga ikiwemo kufungwa taa zaidi ya 30 ambazo ukiingia kila hatua unakutana nazo ambazo zinakuwezesha kuona mbele ili kuwawezesha watalii wa ndani na nje kuweza kuona vizuri uzuri na upekee wa Mapango hayo.

Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Kassim Nyaki ametoa taarifa hiyo wakati wachezaji wa Mamlaka hiyo wanaoshiriki mashindano ya Shimuta walipokwenda kutembelea mapango hayo ambapo alisema wamefanya hivyo kama sehemu ya kufahamasisha utalii wa mapango hayo ya Amboni Tanga.

Ambapo alisema uwepo wa taa hizo unawezesha watalii wa ndani na nje kuweza kuona mbele ambapo watalii wanaofika wanaweza kuona uzuri na upekee wa mapango hayo yaliyosheheni historia mbalimbali zenye kuvutia.

Alisema zamani ulikuwa ukiingia kwenye mapango hayo kipindi cha mvua chini kuna loa kama matope lakini kwa sasa wamepanga matofali kumuwezesha mtalii asipate shida ya kutembelea mapango hayo kipindi cha mvua hivyo kwao ni fursa.

“Vivutio vinavyopatikana madhari tulivu ya mapanga,sehemu ambayo inasemekana mzungu mmoja na mkewe na mbwa walitumbukia na hawajaweza kutokea tena lakini kuna sehemu kuna michoro ya vitabu vya dini kama vile biblia na kiirabu hayo maneneo hayakuandikiwa na mtu ni asili”Alisema Afisa Uhusiano huyo.

Alisema pia kuna sehemu ina ishara ya msikiti na alama  za kanisa kama  eneo lenye muundo wa meli au boti ikiwemo jiwe ambalo limejichonga wenyewe kama tembo huku akieleza wanahamasisha watanzania wote waende kuona upekee na hawatajuta kufika kwenye mapango hayo.

Kabla ya hapo mtu alikuwa akiingia kwenye mapango hayo alikuwa anakutana na giza totoro lakini kwa sasa maboresho yaliyofanywa na serikali ni kuwekwa taa kuna taa zaidi ya 30 zipo ndani ukiingia kila hatua fulani kuna taa ambayo inakuwezesha

Hata hivyo Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro alisema tokea walipokabidhiwa na serikali kuyasimamia mapango hayo kumekuwa na maboresho mengi ambayo yamekuwa na tija.

mapango hayo hivi sasa yapo chini ya Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro na tokea walipokabidhiwa cha kwanza walichofanya kuhakikisha usalama na ulinzi kwenye mapango hayo kutokana na utalii ni starehe .

Alisema lakini silaha ya kwanza katika utalii duniani ni usalama mtu anapokuja watahakikisha anakuwa salama na wapo wamehakikisha eneo lipo salama kila wakati.

“Huko ndani ya Mapango ni eneo kubwa sana inawezekana kunaweza kutokea nyoka hivyo tukaona tufunge taa ambazo mtu akiingia taa zinawaka na kukiwa hakuna mtu kuna kuwa ni kiza ili kutokuathiri uhalisia wa mapango hayo”Alisema

Hata hivyo alisema kinachoendelea hivi sasa ni uwepo wa wahandisi wa Tarura ambao wameshaawaalika wanajenga eneo la kupumzukia wageni na kupata chakula na eneo ambalo litatumika kuweke magari na baada ya wiki  mbili au tatu wataweka mabango.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.