KALIMBA MAGESA KEYYU NDIYE MWALIMU BORA WA SOMO LA KEMIA NCHINI TANZANIA
Mwalimu Kalimba Magesa Keyyu akipokea Kikombe cha Mwalimu Bora wa Somo la Kemia Tanzania |
Kalimba Magesa Keyyu ndiye mwalimu Bora wa Somo la Kemia (Chemistry) kwa Kidato cha Tano na Sita nchini Tanzania.
Tuzo hiyo ya mwaka 2019 ameipat hivi karibuni na Kukabidhiwa Kikombe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI nchini Tanzania Selemani Saidi Jafo,Tuzo hiyo hupatikana kutokana na uchambuzi yakinifu wa matokeo ya Kidato cha Sita kwa mwaka husika ambapo mwaka huu yalitolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania mwezi Julai nchini humo.
Mwalimu Kalimba ambaye pia ni mwimbaji wa Kwaya ya Kanisa la Waadventista ya Njiro jijini Arusha anafundisha katika Shule ya Kidato cha Tano na Sita ya Kisimiri,Arusha ambayo ilikuwa shule ya kwanza kwa matokeo ya Kidato cha Sita nchini Tanzania.
Mwalimu huyo ameieleza mtangazaji.com kuwa Shule ya Kisimiri imekuwa ya kwanza Kitaifa kwa matokeo ya jumla na katika somo la Kemia,yakiwa ni miongoni mwa masomo matatu iliyoongoza kitaifa kwenye matokeo hayo,masomo mengine iliyoongoza kitaifa ni Kiingereza na Historia.
Kalimba anasema kigezo Kikubwa kinachotumika kumpata mwalimu bora ni uwezo wa kuwafanya wanafunzi wa somo hilo kufaulu vizuri katika somo kwa kiwango cha juu ambapo ameeleza kuwa anamshukuru MUNGU kwa kuwa hii ni ya nne kushika nafasi ya kwanza.
Post a Comment