MTANGAZAJI

ADVENTISTHELP NA ADRA WAJENGA HOSPITALI YA KUHUDUMIA WAKIMBIZI MAGHARIBI MWA UGANDA




Taasisi ya AdventistHelp kwa kushirikiana na Shirika la Misaada wakati wa Majanga la Waadventista Ulimwenguni (ADRA) wameungana  kujenga Hospitali katika eneo la Wakimbizi huko Kyaka II Magharibi mwa Uganda.

Kupitia Ukurasa  wa AdventistHelp katika Mtandao wa Kijamii wa Facebook  wameonesha picha za majengo ya Hospitali hiyo iliyoko vijijini yanayoendelea kujengwa ambayo itakuwa ya kwanza ya huduma za dharula za saa 24 katika eneo hilo lenye wakimbizi wapatao 100,000.

Taarifa ya Mpango huo ilitolewa hivi karibuni na miongoni mwa watu wanaojitolea kwa muda mrefu wa taasisi ya  AdventistHelp Dkt  Michael-John von Hörsten katika mahojiano maalum na Shirika la Habari la Waadventista Ulimwenguni (ANN) ambapo amesema eneo hilo linahusika zaidi ya wakimbizi 100,000 toka Kongo wanaokimbia mapigano Mashariki mwa DRC 

Makazi hayo ya wakimbizi yanakadiriwa kuwa na Kilomita 82 yakihusisha nchi tatu za Magharibi mwa Uganda.  
Amesema wanajenga jengo la awali  kwa wagonjwa katika eneo hilo ambalo kuna hitaji la msaada wa masuala ya afya,Jengo hilo ni kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wanaotoka nyumbani kwa kuwapatia huduma ya kwanza,huduma ya meno na mazoezi.

Pia kutakuwa na huduma za dharula ,maabara,utrasound na X-ray ambapo hii itakuwa ni hatua ya kwanza ya ujenzi wa Hospitali hiyo na sehemu ya pili inatarajiwa kuwa ni ujenzi wa jengo la Wodi na chumba cha upasuaji.

AdventistHelp  ilianzishwa mwaka 2015 ikiwa ni kwa ajili ya kusaidia matatizo ya kitabibu  katika jamii kutokana na hitaji lililokuwepo kwa wakimbizi katika eneo la Mashariki Kati wakati huo.Mradi wa kwanza walioshiriki ulikuwa ni msaada wa tiba kupitia vifaa vya tiba vinavyohamishika kwa wakimbizi katika eneo hatarishi la kutoka Uturuki hadi Ugiriki.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.