MTUNZI NA MWALIMU WA KWAYA YA SAUTI YA JANGWANI YA SHINYANGA AFARIKI DUNIA (+AUDIO)
Miongoni mwa Watunzi na Walimu wa Nyimbo wa Kwaya Kongwe ya Sauti ya Jangwani toka Kanisa la Waadventista wa Sabato la Ushirika Mjini Shinyanga Tanzania Mhoja Mambosasa (pichani) amefariki Dunia leo Oktoba Mosi majira ya mchana kwa saa za Tanzania baada ya kile kinachoelezwa kuwa ni kugongwa na Bus la Ally's akiwa anaendesha Pikipiki katika eneo la Station.
Taarifa toka Shinyanga zinaeleza kuwa baada ya ajali alipelekwa katika chumba cha Wagonjwa Mahtuti ICU cha Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga,akiwa njiani kupelekwa Bugando Mwanza walipofika Maganzo ndipo akafariki Dunia.
Mpiga gitaa la Bass wa Kwaya ya Sauti ya Jangwani Daniel Michael na Mwalimu Robert Manyangu ambaye pia ni mpiga gitaa la Solo wa Kwaya hiyo wameeleza kuhusu msiba huo ambapo walizungumzia kwa njia ya Simu na King SemaNaye mwimbaji toka Kahama Shinyanga.

Post a Comment