MTANGAZAJI

EMIRATES WAJA NA KAMPENI YA KULINDA FARU

 
Picha na Matteo Buono

 Shirika la Ndege la Emirates la nchini Dubai limeamua kufanya kampeni ya kuwalinda Faru kupitia michoro ya wanyama hao kwenye ndege zake,kupitia wasifu wa Emirates kwa mtandao wa Twitter wameonesha picha hiyo huku wakieleza kupinga uwindaji na  usafirishaji haramu wa wanyama wakiwemo Faru ili  kuwalinda wanyama hao walio katika hatari ya kutoweka.

Ujumbe huo wa Emirates umeeleza kuwa Faru  wasiozidi 30,000 ndio waliobakia kwa sasa duniani.

Mwaka 2018 Serikali ya Tanzania ilitoa taarifa ya matumizi ya teknolojia kuwafuatilia Faru katika mbuga ya Taifa ya Serengeti ili kukabiliana na uwindaji haramu ambapo Shirika la Hifadhi ya Taifa  Tanzania (TANAPA) lilishiriki katika mpango wa kuweka Faru kifaa cha kidijitali kwenye pembe.

Kifaa hicho kitakuwa kikitoa maelezo kuhusu mwenendo wa Faru maeneo wanamokwenda.
Mradi huo ambao utagharimu dola 111,320 za Kimarekani (Sh253m kwa wakati huo) unatekelezwa kwa ushirikiano wa maafisa wa TANAPA, maafisa wa Shirika la Wanyama la Frankfurt (FZS) na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori ya Tanzania (TAWIRI).

Mradi huo umefadhiliwa na Mfuko wa Uhifadhi wa Friedkin Tanzania (FCF) na hadi Juni mwaka 2018 Faru  21 walikuwa wamewekewa  kifaa hicho kilicho na mitambo ya kisasa zaidi ya kuwafuatilia wanyama, kwa kitaalamu LoRaWAN na hutumia teknolojia ya VHF.
LoRaWAN ni kifaa kidogo sana chenye uwezo mkubwa ambayo huwekwa kwenye pembe za Faru.

Taarifa ya Serikali ya Tanzania ya Julai 2019  kutoka Ofisi ya Rais imesema katika matokeo ya kikosi kazi maalumu kilichoundwa mwaka 2016 kupambana dhidi ya ujangili, idadi ya Faru ambao ni spishi iliyoko katika hatari ya kutoweka, imeongezeka kutoka wanyama 15 tu hadi 167 katika kipindi cha miaka minne.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.