MTANGAZAJI

MAREHEMU MHOJA MAMBOSASA AZIKWA

 

Mwili wa Marehemu Mhoja Mambosasa aliye kuwa Mwimbaji,Mtunzi na Mwalimu wa Kwaya ya Sauti ya Jangwani umezikwa Februari 3 mwaka huu katika makaburi ya Dodoma yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga,Ibada ya kuuona mwili na maziko iliongozwa na Mch Nuhu Suleimani toka Jimbo dogo la Kaskani mwa Ukanda wa Dhahabu katika Kanisa la Waadventista wa Sabato (NGBF) akishirikiana na Kiongozi wa Jimbo la Nyanza Kusini (SNC) Mch Sadoki Butoke,Mch Samweli  Majenga toka Mabatini Mwanza,Mchungaji Kilinda toka Shinyanga na Mch Mhoja wa Mtaa wa Ushirika.

Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na Waumini wa Kanisa la Waadventista,Waimbaji,Wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,ndugu na jamaa toka ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga.

Marehemu Mambosasa enzi za Uhai wake alikuwa Mwimbaji,Mtunzi na Mwalimu wa Kwaya ya Sauti ya Jangwani huku akiwa ni Fundi Sanifu wa Majengo 'mchoraji ramani za majengo' wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhoja Mambosasa (56) alifariki dunia  baada ya kugongwa na Basi la Kampuni ya Ally's Star  eneo la Kituo cha Mabasi ya Kampuni hiyo iliyopo karibu na Stesheni barabara kuu ya Mwanza- Shinyanga akiwa anaendesha pikipiki.
 
Ajali hiyo ilitokea Jumanne ya  Oktoba 1,2019  saba na dakika 50 mchana katika eneo la Ofisi ya Mabasi ya Kampuni ya Ally's iliyopo Mjini Shinyanga barabara ya Shinyanga kuelekea Mwanza.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi alivithibitishia vyombo vya habari  kutokea kwa ajali hiyo.

"Taarifa nilizopewa ni kwamba Mfanyakazi wetu Mhoja Mambosasa ambaye ni fundi sanifu majengo 
alikuwa kwenye shughuli zake kwenye ofisi za Mabasi ya Allys, wakati anatoka kuelekea ofisini akiendesha pikipiki ndipo akagongwa na basi la Allys lililokuwa linaingia kituoni",amesema Mwangulumbi.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi Audax Majaliwa  amesema gari hilo lenye namba za usajili T622 AME aina ya Scania Bus mali ya Yahaya Amor likiendeshwa na Musa Said (40) mkazi wa Mwanza lilimgonga mwendesha pikipiki yenye namba za usajili T843 BBM SANLG aitwaye Mhoja Mambosasa ambaye ni Afisa Mpango miji wa Manispaa ya Shinyanga.
"Mhoja Mambosasa amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga",amesema Kamanda Majaliwa.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari kukata kona kutaka kuingia njia ndogo kutokea njia kuu bila kufuata sheria za usalama barabarani.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.