MAREHEMU MWINJILISTI ELIZABETH BHOKE ALIYEJENGA MAKANISA TANZANIA KUZIKWA OKTOBA 14 MWAKA HUU
Uongozi wa Jimbo la Mara katika Kanisa la Waadventista wa Sabato (MC) kupitia kwa Mwenyekiti wa Jimbo hilo Mch George Ojwang umeeleza kuwa mazishi ya Mwinjilisti Mtaafu Elizabeti Bhoke Babere aliyefariki Oktoba 9,mwaka huu,yatafanyika Oktoba 14 mwaka huu siku ya Jumatatu saa 5:00 asubuhi huko Tambukareli alikokuwa amejenga nyumba yake ya kuishi,Nyumba ya Mchungaji na Kanisa la Mugumu Serengeti jirani na Kisangura alipofia.
Taarifa hiyo ya Mchungaji Ojwang imetolewa kwa viongozi wa Majimbo yote ya Kanisa la Waadventista wa Sabato nchini Tanzania.
Taarifa zinaeleza kuwa Marehemu ambaye alijulikana kwa jina la Bibi Elizabeth Boke ambaye alikuwa Mwinjilisti wa vitabu vya Injili vya Kanisa la Waadventista wa Sabato amelala mauti na hakuwahi kupata mtoto kwa kuwa alifukuzwa na mume wake,inaelezwa alimuomba MUNGU ampe makanisa saba atayojenga ili yawe watoto wake atakaowaacha Duniani na alifanikiwa kujenga makanisa saba na alikuwa akiendelea na la nane hadi mauti ilipompata.
Naye Jackson Silinchah Nyantory toka Mwanza kupitia wasifu wake katika mtandao wa kijamii wa facebook ameandika "Shangazi Elizabeth Bhoke Babele amelala mauti akiwa mstari wa mbele kwa kazi ya Bwana. Ingekuwa jeshini angepewa medali za ngazi ushujaa.
Hata sasa Bwana anajua ametuachia fundisho kubwa kuwa kufanya kazi ya Mungu si lazima uwe tajiri,amejenga makanisa zaidi ya 23 nchini Tanzania lakini alikuwa ni mwinjilisti tu"
Post a Comment