UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU e.V ) UMEFANYA MKUTANO MKUU NA KUCHAGUA VIONGOZI
Umoja
wa Watanzania Ujerumani UTU e.V umefanya mkutano mkuu wa uchaguzi
mjini Aschaffenburg Ujerumani jumamosi 28.09.19.
Katika uchaguzi huo
watanzania wanaoishi Ujerumani walichagua viongozi wapya, nafasi ya Mwenyekiti alichaguliwa Mwl. Bi Upendo Vanessa Lyimo kuwa Mwenyekiti wa
UTU e.V, baada ya mwenyekiti mstaafu Bw. Mfundo Peter Mfundo kukataa
kugombea nafasi hiyo, ambaye amekaa kwa muda wa miaka 9, na kukitumikia
chama hicho kwa muda wote huo, hata hivyo kamati ilimuomba achukue
nafasi ya heshima kuwa mwanakamati, mshauri, mlezi wa UTU e.V na Kiongozi Mwandamizi katika shughuli za UTU e.V
Watanzania wanaoishi Ujerumani waliwachagua viongozi wafuatao.
Mwenyekiti: Mwl. Bi Upendo Vanessa Lyimo
Makamo Mwenyekiti: Bw. Malumbo Salim Malumbo
Katibu: Bi. Petrida Karch
Muweka Hazina: Bw. Mngoya Lukuta
Wanakamati:
Bw. Mfundo Peter Mfundo
Bw. Ebrahim Makunja (aka Kamanda Ras Makunja)
Bw. Sudi Mnette
Post a Comment